Ungependa Nikupatie Mpango Mkakati Na Mbinu Za Kuongeza Mauzo Kwenye Kampuni Yako Kwa BURE?

Kutoka kwa: Mr Bokko (Adelard Ntamaboko)
Dar Es Salaam.
Mpendwa msomaji,
Natafuta kampuni ambayo inahitaji kuongeza mauzo kupitia matangazo ya kulipia mtandaoni ili niisaidie kutimiza lengo hilo haraka iwezekanavyo.
Kama wewe ni mmiliki wa kampuni hiyo, nitafanya kazi pamoja na wewe kukusaidia kuongeza mauzo ya kampuni yako mara mbili, mara tatu au hata mara nne kabisa ya mauzo unayopata kwa sasa.
Hutohitaji kuchukua pesa yako mfukoni kunilipa ili nikusaidie kuongeza mauzo....badala yake nitaongeza kwanza mauzo kwenye kampuni yako halafu utanilipa kutoka kwenye faida ambayo nitakuwa nimeiingizia kampuni yako ndani ya mwezi wa kwanza.
Hii inamaanisha nitafanya kazi ya kuongeza mauzo pasipo kulipwa kwanza. Na endapo nitashindwa kuongeza mauzo sitostahili kabisa kulipwa.
Hata hivyo sidhani kama kuna mtu anaweza akasema kauli hiyo kama kweli hajiamini katika utendaji kazi wake.
Najua unajiuliza mimi ni nani? Na kwanini usikilize ninachokisema?
Nitajitambulisha kwa ufupi kwasababu naelewa haupo hapa kujua historia ya maisha yangu. Upo hapa kwa lengo moja tu – kujua ni jinsi gani naweza nikakusaidia kuongeza mauzo na Faida kwenye kampuni yako.
Kwahiyo, nitajielezea kuhusu mimi kwa ufupi na haraka.
Naitwa Mr Bokko. Mzaliwa wa Kigoma lakini makazi yangu ni Dar es Salaam.
Nilianza kuuza bidhaa mtandaoni kwa mara ya kwanza mwaka 2019.
Bidhaa nilizokuwa nauza ni virutubisho lishe (Food supplements)
Haikuwa rahisi kupata wateja.
Nilijitahidi kwa kadili niwezavyo kutafuta wateja mtandaoni lakini niliambulia kupata wateja 5 tu ndani ya mwaka wangu wa kwanza.
Niliendelea kuhangaika mpaka ikafika hatua nikataka kukata tamaa lakini kabla sijakata tamaa...
Siku moja kwenye pita pita zangu mtandaoni nikakutana na habari za jamaa mmoja wa marekani.
Jamaa huyu anaitwa Vincent James.
Huyu jamaa amewahi kuvunja rekodi kwa kuuza virutubisho lishe na kutengeneza faida ya dola za marekani milioni 100 ndani ya miezi 23 Tu.
Hiyo dola milioni 100 za marekani kwa pesa yetu ya kitanzania ni sawa na Bilioni 200 na milioni 500 ivi.
Fikiria mtu anatengeneza pesa yote hiyo ndani ya miezi 23 tu.
Habari hii kuhusu jamaa huyu ilinivutia zaidi nikaanza kuchimba na kudadisi ni njia ipi anaitumia.
Nilijuwa siwezi nikatengeneza kama hela alizozitengeneza lakini kama nikitumia njia aliyoitumia kuna uwezekano mkubwa na mimi nikaanza kutengeneza milioni kadhaa kila mwezi.
Nilivyomfuatilia huyu jamaa kiundani zaidi niligundua kwamba alikuwa na mfumo ambao ndio ulimwezesha kutengeneza hela nyingi hivyo ndani ya mdu mfupi.
Kwa kutumia mfumo huo alikuwa anapata wateja wapya elfu 40,000 kila mwezi.
Ndani ya miezi 23 akawa tayari kavunja rekodi ya kutengeneza milioni 100 za Marekani.
Basi nikajifunza kila kitu kuhusu mfumo wake nikagundua kwa Tanzania yetu ni ngumu kuutumia kama ulivyo.
Lazima kuwepo na marekebisho ya kuufanya mfumo uendane na Tanzania yetu.
Nikaumiza kichwa ni jinsi gani niufanyie mfumo wake marekebisho ili uendane na Tanzania yetu.
Hatimaye baada ya majaribio ya wiki kadhaa nikafanikiwa kutengeneza mfumo unaoendana na mfumo wa Vincent James lakini ambao unafanya kazi kwa Tanzania yetu.
Pindi nilivyoanza kuutumia mfumo huo, biashara yangu ya kuuza virutubisho lishe mtandaoni ikabadilika moja kwa moja.
Nikaanza kupata mteja wa 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9 sijakaa vizuri ndani ya mwezi wangu wa kwanza nikapata wateja 66.
Hawa ni wateja ambao walinunua bidhaa kuanzia 85,000/= Mpaka 580,000/= na faida yangu kwa mteja mmoja ilikuwa ni asilimia 60% ya bidhaa ambayo mteja anakuwa kanunua.
Kwahiyo faida yangu ilikuwa si chini ya milioni 3.
Baada ya hapo kila mwezi nimekuwa nikipata si chini ya wateja 50.
Nilivyoanza kupata faida nzuri nikajiongeza zaidi... nikaanza kununua program mbalimbali za “Online marketing na Advertising” kutoka kwa mabingwa tofauti tofauti nchini Marekani ili kuongeza maarifa.
Ilivyofika mwaka 2023 mwezi wa 4 nikaamua nisajili na kufungua kampuni yangu ya “Online Marketing System Pro Co LTD” – Kampuni yenye kusaidia wafanyabiashara na wajasiriamali kutafuta masoko kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kampuni yangu kusajiliwa kipaumbele changu kilikuwa ni kusaidia wafanyabiashara kupata masoko ya mtandaoni kwa njia ya wao kujiunga kwenye program zangu za kulipia ambapo nawafundisha kwa njia ya video za online jinsi ya kupata masoko kwenye mitandao ya kijamii kupitia matangazo ya kulipia.

Katika muda wa miezi 6 (Kuanzia 1/5/2023-25/10/2023) mimi binafsi nimetumia bajeti ya 9,290,900/= (Dola 3716.36) katika matangazo ya kulipia mtandaoni kupata wafanyabiashara 342 wa kujiunga kwenye program zangu za kutafuta masoko ya mtandaoni na hivyo kutengeneza jumla ya 34,000,000/=
Kwa lugha rahisi ni kwamba nimepata mara tatu na zaidi ya pesa niliyowekeza kwenye matangazo ya kulipia.
Hii inamaanisha wateja wangu wote nawapata kupitia matangazo ya kulipia mtandaoni.

Picha hiyo hapo juu ni Kwenye account yangu ya Flutterwave kampuni ambayo nimeweka nayo ubia kwa kazi ya kupokea malipo kwenye mfumo wangu ili mtu akilipia hata kama nikiwa nafanya shughuli zingine aweze kupelekwa kwenye mfumo wa mafunzo moja kwa moja.
Jumla ya pesa hapo ni milioni 20 badala ya milioni 34 ni kwasababu wafanyabiashara 7 wamenitumia kila mmoja wao milioni 2 moja kwa moja kwenye account yangu ya Bank ili niwatengenezee mfumo wa kuuza virutubisho lishe.
Najua milioni 34 si kitu kwako ni sawa na pesa ya nyanya tu... hata hivyo lengo langu sio kuonesha kwamba nina hela.
Lengo langu ni kukuonesha kwamba naweza na ninajua kufanya matangazo ya kulipia yenye kuleta faida zaidi ya mara mbili ya bajeti utakayotumia kwenye matangazo yako ya kulipia.
Ni kampuni chache sanaaaa ambazo zinaweza zikaanza leo na zikaanza kutengeneza faida siku ya kwanza kama kampuni yangu.
Hii inamaanisha kama utaniruhusu nishikirie usukani wa mauzo kwenye kampuni yako tegemea mafuliko ya wateja.
Hii Hapa Hatua Ya Kwanza Ya Mimi Kuanza Kuinufaisha Kampuni Yako Kwa BURE!
Kitu cha kwanza ambacho naenda kufanya kwenye kampuni yako ni kukusaidia kutengeneza Mpango mkakati (Plan) wa kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni kupata mauzo na faida ya malengo yako.
Zoezi hili litachukua dakika 30-45.
Huu utakuwa ni mpango mkakati unaoendana na bidhaa au huduma yako.
Baada ya zoezi hili la kutengeneza mpango mkakati wa kuongeza mauzo kukamilika jambo moja kati ya mambo haya 2 litatokea:
- Utaupenda mpango mkakati na kuamua kuufanyia utekelezaji pasipo uhitaji wangu. Kama utaamua hivyo... nakutakia mafanikio mema. Na kama ukipenda unaruhusiwa kunijulisha maendeleo katika utekelezaji wako.
- Utaupenda mpango mkakati na kuniomba uwe mteja wangu nikusaidie kufanya utekelezaji wa kila kitu kwenye mpango mkakati huo.
Hii inamaanisha kila mwezi mimi ndio nitawajibika kurusha na kusimamia matangazo yako ya kulipia mtandaoni kuhakikisha yanaleta faida mara mbili au na zaidi ya bajeti itakayotumika.
Hivi Ndivyo Tutafanya Kutengeneza Mpango Mkakati Wa Kuongeza Mauzo Kwenye Kampuni Yako!
Kwanza kabisa tutafanya mazungumzo ya kwenye simu mimi na wewe kuhusu kampuni yako.
Nitaangalia bidhaa au huduma yako, njia unazozitumia kupata wateja kwa sasa, na malengo yako unayotazamia kutimiza.
Baada ya kujua hizo “malighafi” nitakusaidia kutengeneza mpango mkakati ambao utakusaidia kuongeza mauzo haraka kwa kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni.
Zoezi hili nitalifanya kwa BURE kabisa.
Kwanini Nikupatie Mpango Mkakati Wa Kuongeza Mauzo Kwa BURE?
Kwasababu nikikupatia mpango mkakati wa kuongeza mauzo kwenye kampuni yako utakuwa na machaguo 2.
Moja: Ufanye utekelezaji wa mpango mkakati huo pasipo uhitaji wa msaada wangu.
Kwakua nitakuwa nimekusaidia kutengeneza mpango makakati wa kuongeza mauzo kwa BURE – Hii inamaanisha hata kesho au kesho kutwa ukipata shida yoyote ya kuongeza mauzo mimi ndo nitakuwa mtu wako wa kwanza kuniomba msaada na kuomba tufanye kazi pamoja.
Mbili: Chaguo lako lingine ni hili: Baada ya kukutengenezea mpango mkakati wa kuongeza mauzo unaweza ukahitaji mimi ndo nisimamie na kurusha matangazo yako mtandaoni.
Kama chaguo lako litakuwa hili nitahakikisha mauzo yanaongezeka na faida inakuwa mara mbili au zaidi ya bajeti itakayotumika.
Gharama (ADA) ya mimi kusimamia na kurusha matangazo yako kwa mwezi ni 2,000,000/=
Lakini ukifikiria kuhusu gharama hii utagundua haitakugharimu chochote.
Kwanini?
Kwasababu natalajia kukutengenezea faida ya zaidi ya hiyo 2,000,000/= ndani ya mwezi wa kwanza. Na kama tutaendelea kufanya kazi pamoja kwa miezi 12 mbele, nina uhakika nitaiingizia kampuni yako faida mara mbili au na zaidi ya faida ya sasa.
Hata hivyo... kwa mwezi wa kwanza utanilipa hiyo 2,000,000 baada ya mimi kufanya kazi ya kuongeza mauzo. Hii inamaanisha nitafanya kazi kwanza halafu utanilipa kutoka kwenye Faida ambayo nitakuwa nimeiingizia kampuni yako.
Kama nitashindwa kuongeza mauzo stostahili kulipwa.
Kwahiyo aidha nikupatie mpango mkakati wa kuongeza mauzo kwa BURE na uamue kufanya utekelezaji pasipo uhitaji wa msaada wangu au uamue kuwa mteja wangu nikusaidie kufanya utekelezaji wa mpango mkakati ambao nitakuwa nimekupatia.
Hii ni OFA nzuri ambayo sidhani kama kuna mtu mwingine yeyote kwa hapa Tanzania anaweza akakupatia.
Fikiria kuhusu hilo.
Nakusaidia kukutengenezea mpango makakati wa kuongeza mauzo kwa BURE na kukuacha uamue mwenyewe kuwa mteja wangu ili nikusaidia kufanya utekelezaji wa mpango makakati huo au uamue kufanya utekelezaji pasipo uhitaji wa msaada wangu.
Jumlisha, nimeenda hatua moja zaidi ya kwamba hutanilipa mpaka nifanye kazi yangu ya kuongeza mauzo ndipo unilipe kutoka kwenye faida ambayo nitakuingizia (Kwa mwezi wa kwanza)
Na kama sitaongeza mauzo basi sisitahili kulipwa.
Unahisi nani mwingine mwenye uwezo wa kukwambia hivyo?
Hayupo (Nimefuatilia nikagundua hilo)
Lakini mimi nimeweza kukwambia hivyo kwasababu nina uhakika nitakusaidia kuongeza mauzo.
Hata hivyo...
Huduma hii ninayoitoa Ya kusimamia na kukurushia matangazo yako ya kulipia mtandaoni (Done for you Ads) sio kwa ajili ya kila mtu. Huyu hapa ndiye mtu ninayemhitaji na ambaye naweza nikamsaidia:
Unatakiwa utambue kwamba sina miujiza na wala sitendi miujiza – Maana yangu ni kwamba sina uwezo wa kumsaidia kila mtu. Kwahiyo lazima niseme vigezo anavyotakiwa kuwa navyo mtu ambaye naweza nikamsaidia.
Vigezo hivyo hivi hapa:
1. Unatakiwa uwe na kampuni ambayo tayari inafanya mauzo.
Huduma hii ya kukusaidia kusimamia na kurusha matangazo yako mtandaoni ni kwa mtu ambaye kampuni yake tayari inapata mauzo lakini inahitaji kuongeza mauzo kwa haraka.
Kama kampuni yako ni mpya na hujawahi kuuza bidhaa au huduma yako kabla huduma hii ya usimamizi ninayoitoa sio kwa ajili yako.
2. Unatakiwa uwe na uwezo wa kuwekeza bajeti ya matangazo ya kulipia isiyopungua milioni 3 (3,000,000) kila mwezi.
Kama huwezi ukamudu bajeti hiyo kwa mwezi tafadhali huduma hii sio kwa ajili yako.
3. Lazima uwe na bidhaa au huduma nzuri na ambayo faida yako kwa mteja mmoja ni kubwa.
Ili matangazo ya kulipia yawe ya tija kwako lazima faida unayopata kwa mteja mmoja iwe kubwa kuweza kurudisha gharama zilizotumika kumpata huyo mteja na wewe ubaki na faida yako.
Kama unauza bidhaa au huduma kwa bei ya nyanya hii huduma ya usimamizi sio kwa ajili yako.
4. Lazima uwe tayari kufuata maelekezo nitakayokupatia (Usijali sitakupatia maelekezo ya kipuuzi)
Tazama kama hutafuata maelekezo yangu na kufanya utekelezaji wa kile nitakachokwambia ufanye usimamizi wangu hautakuwa na msaada wowote kwako. Itakuwa haina maana yoyote si ndio?
Hivyo ndio vigezo vyangu.
UNACHOTAKIWA KUFANYA SASA HIVI NI HIKI:
Kama unakidhi vigezo hivyo hapo juu na utapenda nikusaidie kuongeza mauzo nitafurahi kufanya hivyo.
Unatakiwa ufanye “Booking” ya kufanya mazungumzo ya simu na mimi kwa muda wa dakika 30 kuweza kutengeneza mpango mkakati wa kuongeza mauzo.
Kufanya “Booking” ni rahisi.
Bonyeza hapo chini sehemu iliyoandikwa “FANYA BOOKING HAPA”
Baada ya kubonyeza sehemu hiyo utapelekwa kwenye ukurasa mpya ambapo utaulizwa baadhi ya maswali kuhusu bidhaa au huduma yako.
Maswali haya sio magumu. Yanalenga kunipa uelewa wa bidhaa au huduma yako na lengo lako la mauzo unalotazamia kutimiza.
Kama ujumbe huu unauona hewani maana yake bado napokea watu ambao naweza nikawasaidia.
Kuna watu wengi wenye uhitaji wa mimi kusimamia na kurusha matangazo yao mtandaoni.
Sijaajiri bado kwahiyo kazi hii nitaifanya mwenyewe. Hii inamaanisha ikifika idadi ambayo siwezi nikaimudu nitasitisha zoezi la kupokea watu wapya wa kuwasimamia.
Kwahiyo wahi mapema kabla sijasitisha zoezi hili.
Copyright - Online Marketing System Pro