Hii Hapa Hatua Ya Kwanza Kati Ya Hatua 9 Za Kutengeneza Mashine Ya Kukusaidia Kunasa Downlines Wapya Kwa Kufanya Kazi Dakika 60 Tu Kila Siku!

Mambo vipi, Naitwa Mr Bokko. Karibu kwenye darasa hili juu ya hatua 9 za kutengeneza mashine ya kukusaidia kunasa downlines wapya kwa kufanya kazi dakika 60 tu kila siku.
Agenda ya darasa letu ni kama ifuatavyo:
- Darasa hili litachukuwa dakika 5-10 tu kusoma.
- Lengo langu ndani ya muda huo ni rahisi tu. Nimeandika kitabu kipya kinachotoboa siri ya hatua 9 za kutengeneza mashine ya kukusaidia kunasa downlines wapya kwa kufanya kazi dakika 60 tu kila siku. Katika muda huo wa dakika 5-10 nitaelezea nusu ya hatua ya kwanza ya hatua hizi 9. Kwanini nafanya hivyo? Kwasababu sitaki nikutumie kitabu moja kwa moja pasipo wewe kwanza kuona kama kinakufaa kweli.
Kwahiyo, nusu hii ya hatua ya kwanza inatosha kukufanya wewe uamue kama kitabu hiki kinakufaa au hakikufai. Kama utaona kinakufaa basi nitakutumia link ya kukipata kitabu hiki. Na kama utaona hakikufai basi link hiyo itakuwa sio kwa ajili yako.
Ni sawa?
Haya tuanze darasa letu...
Hatua Ya Kwanza!
Elewa upo kwenye biashara gani.
Watu wengi wanajua biashara ni kuuza na kununua. Ndio, ni kweli biashara ni kuuza na kununua. Lakini swali linakuja –unauza nini au unanunua nini?
Jibu la haraka linaweza kuwa bidhaa au huduma.
Vizuri. Kitu kinachouzwa au kununuliwa ni bidhaa au huduma.
Unajua kama kuna watu wanafanya biashara lakini bidhaa au huduma wanayouza sio biashara yao? Watu hawa wapo wengi sana. Na hii ndio sababu kubwa ya biashara nyingi kufa.
Ni ukweli ulio wazi kwamba biashara yoyote ile inahitaji wateja. Lakini ili mteja anunue bidhaa au huduma yako lazima umuuzie bidhaa au huduma anayohitaji yeye na sio unayohitaji wewe.
Tazama –ni rahisi mteja kutoa pesa yake aliyopata kwa shida kukupatia wewe endapo tu unachomuuzia ndicho anachokihitaji yeye.
Na ni ngumu sana mteja kukupatia pesa yake kama unachomuuzia (Kiwe bidhaa au huduma) sicho anachokihitaji yeye.
Kwahiyo, kwasababu ya kutoelewa upo kwenye biashara gani unaweza ukajikuta unawauzia wateja kitu wasichokitaka wao na kujikuta unapoteza wateja kila siku.
Kama nilivyokwambia biashara nyingi zinakufa kwasababu ya wafanyabiashara wengi kutojua wapo kwenye biashara gani.
Matokeo yake wanajikuta wanawauzia bidhaa au huduma ambayo wateja hawahitaji kununua.
Kwa mfano: unadhani mpiga picha biashara yake ni nini?
Nilijua tu lazima useme biashara yake ni kupiga watu picha.Hapana sio kweli. Biashara yake sio kupiga watu picha.
Biashara yake ni nini sasa? Biashara yake ni kuwauzia watu umuhimu wa kutunza kumbukumbu ya matukio.
Tazama –watu wanapiga picha kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya matukio yaliyopita. Hivyo basi, kama mpiga picha, biashara yako ni kuwauzia watu umuhimu wa kuwa na kumbukumbu ya matukio ya nyuma.
Unahisi itakuwa ni rahisi au vigumu mtu kupiga picha endapo mpiga picha atamuelezea mtu huyu umuhimu wa kutunza kumbukumbu? Lazima iwe rahisi mtu huyu kupiga picha kwasababu anachouziwa ndicho anachokihitaji.
Sasa, utakuta wapiga picha karibia wote wanachokiuza kwa wateja ni ubora wa picha na takataka zingine kibao.
Mara ngapi umekutana na mpiga picha aliyesisitiza juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu? Mimi binafsi sijawahi kukutana nae hata mmoja.
Ndio maana nimekwambia biashara nyingi sana zimekufa na nyingine nyingi zitazidi kufa kwasababu wafanyabiashara hawaelewi wapo kwenye biashara gani.
Nisikilize kwa makini –biashara yako sio bidhaa au huduma yako. Biashara yako ni kile ambacho bidhaa au huduma yako inaenda kufanya.
Sasa, turudi kwenye network marketing; Kama networker unadhani wewe biashara yako ni nini?
Usinifanye nicheke. Umesema?
Yaani licha ya kukwambia biashara yako ni kile ambacho bidhaa au huduma yako inaenda kumfanyia mteja lakini bado umeshindwa kujua upo kwenye biashara gani.
Nakupatia nafasi nyingine tena ya kujaribu.
Upo kwenye biashara gani?
Unaona –si ajabu ni ngumu sana kwako kupata downlines wapya kwasababu hata huelewi upo kwenye biashara gani. Matokeo yake unajikuta unawauzia prospects wako kitu ambacho wao hawakihitaji.
Sogea karibu nikwambie kitu: Biashara yako sio kuingiza watu kwenye fursa na wala sio kuuza bidhaa za kampuni uliyopo.
Ona –kwa networker asiyejua yupo kwenye biashara gani atajikuta kila siku anasifia ubora wa mfumo wa malipo na bidhaa za kampuni ambayo hata sio yake.
Hivi unadhani kampuni uliyopo ni yako? Sidhani kama unafikiria hivyo. Kama unafikiria hivyo naomba ubadili fikra zako kuanzia sasa hivi.
Kampuni uliyopo sio yako rafiki yangu. Wewe ni dalali tu ambaye unalipwa ukiingiza mtu kwenye fursa au ukiuza bidhaa zao. Au kwenye kampuni uliyopo unalipwa hata kama hujauza au hujaingiza mtu kwenye fursa?
Achana na habari za kulipwa kupitia kazi iliyofanywa na downlines wako. Ninachokimaanisha ni kulipwa pasipo wewe au downlines wako kufanya mauzo yoyote au kuingiza mtu yeyote kwenye fursa?
Sidhani kama kampuni hiyo ipo hapa duniani. Ili ulipwe kwenye biashara hii ya network marketing lazima uuze bidhaa au uingize watu kwenye fursa.
Kwahiyo, yakupasa uelewe kwamba kampuni uliyopo sio biashara yako. Kama ukilitambua hilo nina uhakika tayari unajua biashara yako ni nini, si ndio?
Acha kuniangusha. Yaani licha ya maelezo yote hayo niliyokupatia bado hujui biashara yako ni nini?
Haya kama bado hujajua biashara yako ni nini ngoja niendelee kukuelezea mpaka pale ubongo wako utakapofunguka.
Hapo juu nimekwambia wewe ni dalali ambaye unalipwa pale ambapo umeuza bidhaa au umemuingiza mtu mpya kwenye fursa.
Sasa, nikuulize swali –mtu anapojiunga kwenye fursa anajiunga kwako wewe au kwenye kampuni?
Jibu lipo wazi. Anajiunga kwako wewe. Na ndio maana kampuni inakulipa wewe kwa kumuingiza mtu huyo mpya.Kwahiyo, yakupasa ujue kwamba watu wanajiunga kwa watu na sio kwenye kampuni.
Sasa, kama anajiunga kwako wewe unahisi mtu huyu kitu ambacho kitamfanya yeye ajiunge kwenye hiyo fursa ni kampuni au ni wewe?
Jibu lake tena lipo wazi –ni wewe.
Sasa, kama mpaka mtu anajiunga kwenye fursa kinachoangaliwa ni wewe unahisi biashara yako ni nini?
Ngoja nikusaidie rafiki. Biashara yako wewe kama networker ni WEWE!
Wewe ndio bidhaa ambayo prospects wanayoinunua pale wanapoamua kujiunga kwenye fursa.
Angalia –mpaka mtu anajiunga kwenye fursa hakuna sehemu ambapo kampuni itakuja ikusaidie kuhakikisha mtu huyu anajiunga kwenye fursa. Kampuni inasubiria umuingize ndipo wao wakulipe wewe dalali wao pesa yako.
Kwahiyo sasa, mtu anapojiunga kwenye fursa –kilichomfanya ajiunge kwenye fursa sio kampuni bali ni wewe. Hivyo basi, yakupasa utambue kwamba wewe ndio bidhaa ambayo prospects wanainunua.
Ukiwa kama bidhaa ambayo prospects wanainunua ndio wajiunge kwenye fursa, biashara yako ni kuuza ubora wako wewe na sio ubora wa mfumo wa malipo au bidhaa.
Kutangaza ubora wa mfumo wa malipo na uzuri wa bidhaa sio biashara yako. Hiyo ni biashara ya wenye kampuni ili kupata madalali kama wewe wengi. Wewe biashara yako ni kuwa bora kiasi kwamba mtu atatamani awe na wewe kwenye fursa yako.
Swali ambalo unatakiwa ujiulize ni kwamba...
Hapo ndo mwisho wa nusu ya Hatua ya Kwanza. Nina Imani mpaka hapo unajua kama kitabu hiki kinakufaa au hakikufai. Kama unahisi kinakufaa link ya kukipata hii hapa chini. Bofya kwenye "Nitumie Kitabu Changu"
Copyright - Online Marketing System Pro