Utangulizi Wa Challenge Me In 7 Days!

Kabla Ya Challenge Kuanza Tazama video Hizi 4.

UTAJIFUNZA NINI KUTOKA KATIKA KILA VIDEO??

Kupata maelezo mafupi kuhusu utakachojifunza kwenye kila video bonyeza kwenye kipembe 3 kidogo kilichopo mwisho wa video husika hapa chini.


Ukimaliza kusoma maelezo mafupi ya video husika bonyeza tena kwenye kipembe 3 kuweza kufunga maelezo hayo ili ubonyeze kwenye kipembe 3 cha video inayofuata kupata maelezo yake mafupi.

Video 1

Video ya kwanza Inahusu Sababu 7 Zinazosababisha Watu Wasifanikiwe Mtandaoni.


Sababu hizi ni kama makosa ambayo watu wanayafanya mtandaoni na mwisho wa siku kujikuta hawafanikiwi na kushindwa kutimiza malengo yao.


Ni muhimu sana kuyatambua makosa haya kwasababu itakuwa rahisi kwako kuyaepuka ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufanikiwa na kutimiza malengo yako.


Baada ya kuwa na uelewa wa makosa haya sasa nakukaribisha kwenye video ya pili.

Video 2

Video ya pili inahusu chimbuko la mfumo wangu ninaotumia kunasa wateja wengi mtandaoni.


Mfumo huu haukushushwa kutoka mbinguni ukaingia kichwani mwangu. Nilifundishwa na walionitangulia kwenye masuala ya marketing ambao ni Mentors wangu kutoka Marekani.


Ni muhimu kuelewa chimbuko la mfumo wangu kwasababu na wewe unaweza pata wazo la kuanzisha mfumo wako hata kwa hapo badae.


Baada ya kuelewa chimbuko la mfumo wangu nakukaribisha kwenye video ya 3 ambapo naelezea jinsi nilivyofanya uboreshaji kutoka kwenye chimbuko na kuzalisha mfumo wangu ambao unaendana na Tanzania Yetu.

Video 3

Video ya tatu inahusu mfumo wangu wa kunasa wateja.


Kwenye video hii nitakuonesha safari ya mtu kuanzia pindi anapoingia kwenye mfumo wangu kwa kuona Tangazo langu mtandaoni mpaka kwenye hatua ya mwisho ambapo mtu huyu anajaza fomu ya kuweka ODA ya kuchukuwa bidhaa akiwa tayari kaipenda bidhaa na anajua bei yake kabla ya kuongea na wewe.


Baada ya mtu huyu kuweka ODA unatumiwa ujumbe kwenye barua pepe (email) yako kwamba kuna mtu kaweka ODA.


Baada ya hapo nakukaribisha kwenye video ya mwisho.

Video 4

Video ya 4 inahusu Namna Sahihi ya kuzungumza na mteja ambae anakuwa kaweka ODA ya kuchukuwa bidhaa.


Kwenye video hii nitakufundisha jinsi ambavyo inatakiwa uzungumze na mteja alieweka ODA na kujibu baadhi ya maswali yake atakayokuuliza.


Baada ya hapo kama utakuwa na swali au maswali yoyote kuhusu video hizi nenda kwenye group uliza maswali hayo nitakujibu.


Kama hauna swali lolote hatua inayofuata nikuanza challenge yetu. Ili nijue upo tayari kwa challenge post kwenye group neno "Nipo tayari kwa challenge"

Sasa Tazama Video Moja Baada Ya Nyingine Kwa Kufuata Mpangilio Wake Hapa Chini.

sasa unaitazama:

 Video 01 

SASA UNAITAZAMA:

 Video 02 

SASA UNAITAZAMA:

 Video 03 

SASA UNAITAZAMA:

 Video 04 

>
error: Copying is not allowed on this website
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications