Hatua ya #1: Angalia Video Hii Mpya Inayofichua Makosa Makubwa Yanayosababisha Usipate Watalii na Ugundue Mbinu Zinazotumiwa na Tour Operators Kutoka Ufaransa, Ugiriki, Ufilipino, na Thailand Kupata Watalii Ndani Ya Masaa 48 Kwa Kutumia Matangazo Ya Kulipia!

Hatua ya #2: Soma Ujumbe Huu


Ndugu Tour Operator,


Kama wewe ni mkongwe kidogo kwenye biashara ya utalii, nina imani umejiunga na madarasa mengi ya jinsi ya kufanya matangazo ya kulipia Facebook na Instagram, lakini bado changamoto ya kupata watalii iko pale pale!


Ninalijua hili kwa sababu, mwaka 2023 mwezi wa tano, nilitoa programu moja inayoitwa “Facebook & Instagram Mapene,” ambayo ililenga kufundisha wafanyabiashara mbinu ya Targeting Hack—njia ya kugundua mamia ya interests ambazo, ukizilenga, unapata faida kubwa kwa bajeti ndogo.


Wafanyabiashara 558 walijiunga kwenye programu hii.

Wapo waliojiunga kwa bei ya 80,000, wengine kwa 55,000, na wengine kwa 35,000.


Wafanyabiashara wengi sana waliipenda programu hii, na kwa kweli, iliwasaidia sana.


Miongoni mwa wafanyabiashara hao waliojifunza kutoka kwenye programu hii walikuwa ni pamoja na Tour operators.


Lakini sasa, je, Tour operators hao walifaidika na mafunzo haya?


Ngoja niwe mkweli na muwazi:

Ukweli ni kwamba walifaidika kidogo sana. Wapo walionipigia simu wakisema wamepata mwanga, lakini shida yao ya kupata watalii ilibaki pale pale.


Sababu kuu kwanini programu hiyo haikuwasaidia sana ni kwamba mafunzo yake yalilenga biashara zinazolenga wateja wa ndani, yaani Watanzania. Lakini, kwenye biashara ya Utalii, walengwa ni watu kutoka nchi za Ulaya, Canada, na Marekani.


Sasa, kurusha matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kwa ajili ya watu wa Ulaya, Canada, na Marekani ni tofauti kabisa na jinsi unavyorusha matangazo yanayolenga Watanzania.


Nitakufafanulia utofauti huo mbele kidogo, lakini kwa sasa ngoja nikuambie kilichotokea baada ya baadhi ya tour operators kunipigia simu wakihitaji msaada zaidi.


Kusema ukweli, kwa wakati ule sikuwa na msaada wowote wa kuwapa tour operators kwa sababu sikuwa na mbinu za kuliteka soko la kitalii la Ulaya, Canada, na Marekani.


Kwa hiyo, niliendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara ambao soko lao ni la ndani, Tanzania. Nikaanzisha programu nyingi ambazo zote zilienda kuwa “Best Sellers.” Wafanyabiashara wengi walipenda mafunzo hayo na bado wanayapenda kwa sababu yalibadilisha biashara zao.


Ilipofika mwezi wa 10 mwaka 2023, nilipata wazo la kuingia kwenye soko la Ulaya, Canada, na Marekani.


Wazo langu lilikuwa kufanya “High Ticket Affiliate Marketing” — kuuza bidhaa za thamani kubwa ambazo zinagharimu $1997 hadi $5000, ambapo mimi nalipwa asilimia 40%–60% ya mauzo.


Kwa mbinu nilizokuwa nazo hapo awali, nisingeweza kufanikiwa kwenye biashara hii. Kwa hiyo, niliamua kununua kozi moja ya $2497.


Kozi hiyo ilifundisha mbinu zote za kuuza bidhaa yoyote ya bei kubwa kwenye masoko ya Ulaya, Canada, na Marekani.


Miongoni mwa yaliyofundishwa kwenye kozi hiyo, kulikuwa na kipengele cha “The Tourism Funnel” — mbinu za kuuza package za utalii kupitia matangazo ya kulipia.


Kwa kuwa lengo langu la kununua kozi hiyo lilikuwa kujifunza “High Ticket Affiliate Marketing,” hicho kipengele cha biashara ya utalii sikukitilia maanani sana. Nikaamua kuachana nacho!


Kwa miezi kadhaa, nimekuwa bize na biashara ya ‘High Ticket Affiliate Marketing’ mpaka siku moja aliponipigia simu tour operator mmoja, akiniuliza kama natoa mafunzo ya jinsi ya kupata watalii kupitia matangazo ya kulipia kwenye Facebook na Instagram.


Kwa kuwa miezi kadhaa ilikuwa imepita tangu niliponunua programu ya ‘High Ticket Affiliate Marketing,’ nilikuwa nimeshasahau kama kuna kipengele kinachofundisha hatua zote za kuuza package za utalii.


Hata hivyo, baada ya simu ya huyo tour operator, kumbukumbu zilirudi. Nilirudi kwenye hiyo course na kupitia kwa kina kipengele cha ‘The Tourism Funnel.’


Katika kipengele hicho, kuna case studiesreviews, na shuhuda nyingi kutoka kwa tour operators wa Thailand, Ugiriki, Ufaransa, Ufilipino, na nchi zingine kibao.


“The Tourism Funnel” ni njia Mpya, ya Kipekee na Ambayo Hujawahi Kuiona Au Kuisikia Sehemu Yoyote Ile!”


Baada ya kuona tour operators kutoka nchi zingine wakisifia njia hii na kutoa shuhuda za matokeo wanayopata ndani ya muda mfupi, nilikumbuka kuwa tour operators wengi wa Tanzania bado wanahangaika kupata njia sahihi na ya uhakika ya kupata watalii. Hivyo, nimeamua kuanza kutoa huduma hii ya kuwatengenezea "The Tourism Funnel"

Hatua ya #3: Tufanye Mazungumzo Tuone Jinsi Gani Naweza Nikakutengenezea "The Tourism Funnel"


Kama umemaliza kuangalia video hiyo hapo juu na umesoma ujumbe huo hapo juu, bonyeza "Naomba Tuwasiliane" ili tufanye mazungumzo ya lini nianze kukutengenezea kila kitu nilichokifundisha kwenye video!

© 2026, Online Marketing System Pro

This site is not a part of the FacebookTM website or FacebookTM  Inc. Additinally, this site is NOT endorsed by FacebookTM  in any way. FACEBOOKTM is a trademark of FACEBOOKTM, inc.

>
error: Copying is not allowed on this website
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications