Kila mbinu mpya niliyojifunza nilijaribu kuona kama ingekuwa na manufaa kwangu.
Nilijifunza mengi kuhusu matangazo ya kulipia Facebook na Instagram lakini taarifa mbaya ni kwamba niliishia kupoteza hela nyingi kuwalipa Facebook na Instagram bila kupata matokeo mazuri.
Ndani ya mwaka mmoja niliishia kupata wateja 5 tu.
Funzo ambalo unatakiwa ulipate hapa ni kwamba...
Usifanye matangazo ya kulipia Facebook au Instagram kama hujui unachokifanya ni nini maana kwa vyovyote vile utaishia kupoteza hela zako ambazo bora hata ungetoka zako mtoko ukapunguza msongo wa mawazo.
Usije ukawa kama wengi wanachokifanya kubandika Tangazo na kuanza kufanya maombi na kutumaini kupata wateja wengi.
Huo ni wehu na uchizi. Kama hujui unachokifanya kuhusu matangazo ya kulipia acha kabisa utapoteza hela nyingi.
Nini kilichotokea baada ya kupoteza hela nyingi kwenye matangazo ya kulipia?
Siku zote huwa kuna njia sahihi na pekee ya kufanya jambo fulani kwahiyo, sikukata tamaa nikaendelea kujaribu kila nilichokiweza lakini mwisho wa siku nikaona pengine biashara hii sio kwa ajili yangu. Nikawaza kuachana nayo ili nifanye mambo mengine.
Lakini kabla sijaamua kuacha biashara rasmi nikapata wazo la kufanya utafiti kwanza.
Utafiti wa kujua kama kuna njia nyingine ya uhakika wa kupata wateja kwa kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram.
Siku moja katika tafiti zangu nasoma makala hii inayomzungumzia jamaa mmoja wa marekani anayepata wateja wapya kila mwezi zaidi ya 500 kupitia Matangazo ya kulipia Facebook na Instagram.
Najiuliza...
“Hii inawezekanaje?”
Yani mimi hapa napambana kwa nguvu zote. Nafanya kila ninachofundishwa. Naishia kupata wateja 5 tu ndani ya mwaka mzima halafu hapa kuna mtu ndani ya kila siku 30 anapata wateja wapya zaidi ya 500.
Haikuniingia akilini kabisa.
Ikabidi niendelee kufanya udadisi wa kujua jamaa huyo anatumia mbinu gani kupata wateja wapya zaidi ya 500 kila mwezi.
Nilifanya udadisi mpaka nikajua kila kitu alichokuwa akikifanya.
Jamaa huyu alijua mbinu sahihi na ya kipekee ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata mafuliko ya utitiri wa wateja.
Nikajifunza kila kitu kuhusu mbinu hii na baada ya hapo mbinu hii imebadili maisha yangu na biashara yangu mazima.
Haya hapa Matokeo Niliyoyapata Baada Ya Kujifunza Mbinu Hii Kutoka Kwa Huyu Jamaa Wa Marekani.
Nilivyomaliza mafunzo nilikuwa kwenye kipindi cha kuelekea kuwa na maisha ya ndege yaani kukosa sehemu ya kuishi kwa kushindwa kulipa kodi.
Zilikuwa zimebaki siku 9 tu mwenye nyumba aje adai chake. Na mwenye nyumba alikuwa hataki masihara kabisa kwenye suala la kulipa kodi. Usipolipa kodi kwa wakati anakutimua. Kwahiyo nilikuwa na mambo 2 ya kufanya. Nipate hela ya kodi ndani ya siku hizo 9 au nisubiri kutimuliwa nianze maisha ya ndege.
Kipindi hicho nilikuwa nakaa nyumba ambayo kodi nilikuwa nalipa 120,000/= kwa mwezi. Kwa mahesabu ya haraka ndani ya siku 9 nilikuwa nahitajika niwe na 720,000/= (Kodi ya miezi 6)
Mfukoni nilikua na 100,000/= tu. Kwa mbinu ya kupata wateja ambayo nilikuwa nimejifunza tayari, hiyo laki moja nikaamua niitumie kama bajeti ya tangazo nililoliandaa.
Nikaandaa kila kitu kilichohitajika kunipatia wateja wengi. Baada ya hapo nikabandika tangazo lionekane facebook na Instagram kwa bajeti ya dola 3 kila siku.
Kuifupisha stori baada ya siku 9 kufika nilikuwa nimeshaingiza faida ya 1,200,000/= Nikalipa kodi na bado nikabaki na pesa za matumizi.
Kumbuka bajeti ya tangazo ilikuwa ni dola 3 kila siku, kwa muda wa siku 9 ilikuwa jumla dola 27 (Sawa na 66,000/=). Kwahiyo nilitumia 66,000/= kuzalisha faida ya 1,200,000/= ndani ya siku 9 tu.
Hapo ndipo nilipojua nimepata fomula ya kufanya matangazo ya kulipia Facebook na Instagram yanayoleta mafuliko ya wateja kwa bajeti ndogo na ndani ya muda mfupi.
Baada ya hapo kuuza kwangu kumekuwa kama kunywa maji. Nikiamua kuuza kweli natengeneza mpaka faida ya 5,000,000/= ndani ya mwezi mmoja.
Hesabu zangu zinanionesha kwa sasa faida ya mauzo yangu kwa mwezi si chini ya 3,000,000/=
Si hivyo tu...
Mwezi wa 8 mwaka 2022 niliweka lengo la miezi 4 (wa 8, 9,10 na 11). Lengo lilikuwa ni kwamba kwa kila faida ya mauzo nitakayoipata 2,500,000 inabidi niiweke kwenye account yangu ya Bank na nyingine iliyobaki ndio nifanyie mambo yangu mengine.
Je lengo hilo lilitimia?
Tazama kwenye picha hizi 2 hapa chini.
Unaweza ukaona mwenyewe kwamba lengo lilitimia. Lakini kumbuka mimi ndo yule ambae ndani ya mwaka mzima nilipata wateja 5 tu kabla sijajifunza mbinu hii ninayoitumia kwa sasa.
Kwahiyo haijalishi biashara yako ipo kwenye hali gani kama utaniruhusu nikufundishe mbinu hii nakuhakikishia utafulikwa kwa utitiri wa wateja kwa bajeti ndogo na ndani ya muda mfupi.
Tazama, nimekuwa nikitumia mbinu hii kwa zaidi ya mwaka na miezi kadhaa. Kwahiyo nina uhakika kabisa 100% ukiijua mbinu hii lazima watu waliokuwa wanakuchukulia poa wakukome maana utaanza kuuza si kawaida.
Lakini ningependa nikwambie kitu kimoja ambacho kinaweza kikakuvunja moyo usitake nikufundishe mbinu hii.
Kitu hicho ni hiki...
Nimekuwa nikiitumia mbinu hii siku zote na imekuwa ikinipatia matokeo makubwa sana kwa kila tangazo ambalo narusha Facebook au Instagram.
Lakini ilivyofika...
Mwezi wa pili mwaka huu (2023) mambo yakaanza kuwa tofauti.
Nilikuwa na matangazo 5 tofauti ambayo yalikuwa yapo “active”.
Bajeti ya kila tangazo moja kwa siku ilikuwa ni dola 10 (sawa na 24,500/=) Kwahiyo kwa matangazo yote 5 jumla ya bajeti kwa siku moja ilikuwa ni dola 50 (sawa na 122,500/=)
Kabla ya mwezi wa pili kufika, matangazo hayo yalikuwa yananiletea wateja wengi sana kama utitiri.
Ilikuwa haipiti siku sijatengeneza faida si chini ya 250,000/=
Lakini ilipofika mwezi wa pili tu matangazo hayo yakaanza kuwa hasara.
Siku ya kwanza ikapita sijatengeneza faida yoyote nikaishia kupata hasara ya dola 50 ambayo ndio bajeti ya matangazo yote 5 kwa siku moja.
Nikaamua nizime matangazo 4 libaki moja tu nione itakuaje.
Siku ya pili ikapita kimyaaaa hakuna mteja hata mmoja nikaishia kupoteza dola 10 ambayo ilikuwa ni bajeti ya tangazo hilo moja.
Kumbuka hapo nishakula hasara jumla ya dola 60. Siku ya kwanza kwa matangazo 5 hasara ya dola 50 na siku ya pili kwa tangazo moja dola 10 kwahiyo jumla dola 60. (Sawa na 145,200/=)
Uvumilivu ukanishinda nikaamua na hilo tangazo moja nilizime kwanza.
Nikaanza kupata msongo wa mawazo nini nifanye maana hela zote ninazozitengeneza ni kupitia matangazo ya kulipia kwa mpenzi Facebook na Instagram.
Sasa matangazo hayaleti faida tena nifanyeje?
Zikapita siku kadhaa nawaza na kuwazua nifanyeje.
Nikaamua kuandika matangazo 2 mapya. Nikawa na uhakika kabisa lazima nitaanza kufulikwa na wateja kwa mara nyingine tena.
Matangazo hayo 2 nikaweka kila moja dola 5 kwa siku.
Siku ya kwanza ikapita kimyaaaaaaaaaa. “No” mteja. Hasara ya dola 10 nyingine hiyo kwa hayo matangazo 2.
Nikasema ngoja nisikilizie siku ya pili nione itakuaje.
Siku ya pili ilipofika nikayazima hayo matangazo 2 maana yaliongezea hasara ya dola 10 nyingine.
Kwahiyo mpaka muda huo nikawa na hasara jumla dola 80 (sawa na 193,600/=)
Kuna mtu hapa unasema unakubalije kupoteza hela yote hiyo kizembe.
Jibu ni rahisi...
Hata kama wewe ni mzoefu wa matangazo kiasi gani, kuna siku tu itafika matangazo yataacha kukuletea faida.
Sasa siku hiyo ikifika endapo hujui ni nini ufanye lazima utaishia kupoteza hela kama kilichonitokea.
Kwahiyo nilipata hasara kwasababu sikujua chakufanya pindi tatizo hilo la matangazo kuacha kuleta matokeo linapotokea.
Nilijaribu kila nilichokiweza mpaka ilipofika hasara ya dola 91 (Sawa na 220,220/=) nikaamua nisifanye tangazo lolote mpaka nitakapopata suluhisho la changamoto hiyo.
Siku moja Katika pitapita zangu Facebook nikaona Tangazo kutoka kwa jamaa mmoja wa Nigeria anayeishi Marekani.
Tangazo hilo lilikuwa linasema kwamba jamaa anauza “Course” ambayo inatoboa siri ya mbinu ambayo inatumiwa na manguli kama...
Mbinu aliyokuwa anafundisha ni kutumia “Targeting Hack” kugundua makundi ya watu Facebook na Instagram ambayo hakuna mfanyabiashara mwingine anayajua bila kutumia hii “Targeting Hack”. Kwahiyo ukiyajua makundi hayo maana yake wewe pekee ndio utaweza kuwalenga na kuwaonesha matangazo yako na hivyo kufanya ujiondoe kwenye ushindani na kutengeneza faida kubwa kwa bajeti ndogo na ndani ya muda mfupi.
Course hiyo inauzwa kwa dola 297 (Sawa na 718,740/=) lakini muda huo nilipoona Tangazo hilo alikuwa katoa punguzo la bei mpaka dola 47 (Sawa na 113,740/=)
Bila kuchelewesha nikanunua “Course” hiyo kwa hiyo 113,740/=
Kabla sijatulia vizuri akanipatia OFA nyingine ya masaa 72.
Akaniambia ana “Course” Ambayo inafundisha kila kitu kuhusu Kutangaza biashara yoyote Facebook au Instagram ambayo anaiuza kwa dola 997 ( Sawa na 2,422,710/=). Lakini ndani ya masaa 72 ananipunguzia mpaka dola 299.9 (Sawa na 730,200/=)
Weeee nikasita kununua. Sio kwamba sikuwa na hiyo hela. Kumbuka mpaka mimi kununua hiyo "Course" ya kwanza ni baada ya matangazo yangu ambayo yamekuwa yakiniingizia faida kuanza kuleta hasara. Kwahiyo nilichokihitaji kwa wakati huo ni njia ipi niitumie kufanya matangazo yangu yaanze kuniingizia faida tena kama mwanzo. Kwakua "Course" ya kwanza ilikuwa inahusu njia hiyo basi nikaona ni vyema kwanza nitatue tatizo langu kuliko kuwaza "Course" ya pili inayofundisha jinsi ya kutangaza aina yoyote ile ya biashara mtandaoni.
Nikajipa siku 3 nikasema ngoja nijaribu kwanza nitakachojifunza kwenye “Course” ya kwanza ikiwa matangazo yangu yataanza kuniletea matokeo tena kama mwanzo basi faida nitakayoipata ndio nitaongezea ninunue “Course” hiyo ya pili ili niongeze maarifa zaidi kuhusu kupata wateja mtandaoni.
Nikatumia “Targeting Hack” kugundua makundi mapya ya watu Facebook na Instagram ambayo watu wachache tu wanaofahamu mbinu hii ndio wanayajua.
Nikachukua matangazo 2 kati ya yale matangazo 5 ambayo yalikuwa yameacha kuniletea matokeo.
Sikubadili hata nukta kwenye matangazo haya.
Nilikopi na kupesti kama yalivyo isipokuwa utofauti ulikuwa kwenye watu ambao watayaona matangazo hayo.
Kwakuwa nilikuwa tayari nimegundua makundi mapya niliweka dola 10 kama bajeti ya kila siku kwa kila Tangazo kwa hayo matangazo 2.
Ngoja tuone matokeo yake:
Siku ya kwanza tu nilitengeneza faida ya 510,000/= Hiyo ni faida baada ya kutoa bajeti (Dola 20 sawa na 50,000/=) iliyonisaidia kupata faida hiyo pamoja na bei ya bidhaa. Nimepiga mahesabu juu kwa juu sijataka tuanze kupoteza muda.
Au kwa maelezo rahisi ni kwamba siku ya kwanza nilitumia bajeti ya 50,000/= kwa matangazo yote 2 kuzalisha faida ya 510,000/=
Siku ya pili nikatengeneza Faida ya 246,000/=
Siku ya tatu nikatengeneza faida ya 826,000/=
Sitaki niendelee siku ya 4 ilikuwaje tuishie hapo siku ya tatu.
Kwahiyo kwa siku hizo tatu tu nilitengeneza jumla ya 1,582,000/= kama faida.
Tazama...course iliyonipatia mbinu ya kupata faida hiyo nilinunua kwa 113,740/=
Kwahiyo kwa lugha rahisi ni kwamba nilimpa jamaa 113,740/= halafu yeye akanipatia 1,582,000/= na zaidi kwasababu mbinu hiyo bado itaniingizia faida tena na tena sijui mwisho wake lini.
Tusisahau ile OFA ya masaa 72 ambayo nilipewa badala ya kulipa dola 997 nilipe dola 299.9
Kwakua nilikuwa tayari nimetatua changamoto yangu na kupata matokeo makubwa kutoka kwenye course ya kwanza nilikuwa na mzuka wa hali ya juu wa kutoa hiyo dola 299.9 maana nilijua kutoka kwenye course hiyo ntakuwa nimenunua tiketi ya kugundua siri nyingi za kupata wateja mtandaoni ambazo watu wengi hawazijui.
Bila kuchelewesha unaweza ukaona kwenye screenshot hapa chini tarehe 17 mwezi wa 2 mwaka huu wa 2023 nikaamua kununua course hiyo.

Sikuishia hapo. Usiku wa Sikukuu ya Pasaka wakati wengine wanasherehekea kwa namna yao na mimi nikaamua nisherehekee kiana yake.
Kwa siku nyingi nimekuwa nikitamani kuwa mwanafunzi wa nguli mmoja ambae namkubali sanaaaaaa. Nguli huyu Ni wa Marekani. Anaitwa Frank Kern. Huyu jamaa ni hatari sana kwa Online marketing & Advertising.
Basi usiku huo wa pasaka nikaamua ninunue "Course" moja kutoka kwake inayohusu namna ya kuifulika biashara yako kwa utitiri wa wateja hata kama wewe ni mpya kwenye biashara.
Course hiyo ilikuwa inauzwa kwa punguzo la bei dola 397 (Sawa na 973,163/=)
Kama kawaida yangu nikiona punguzo la bei huwa sicheleweshi kufanya maamuzi. Unaweza ukaona kwenye screenshot hapa chini.

Baada ya kununua course hizi nimegundua Watanzania wengi sanaaa hasa wafanyabiashara na wajasiriamali kuna vitu vingi sana hawavijui kuhusu kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi kama utitiri.
Kusema ukweli sikuwa na mpango wowote wa kumfundisha mtu yeyote mbinu hizi, lakini kulingana na hali ya kusumbuliwa na watu wengi kutaka kujua mbinu ninazozitumia nikaona kumfundisha mtu mmoja mmoja nitajichosha BURE.
Kwahiyo nikaona njia rahisi na pekee ya kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali wengi ni kuandaa darasa ambalo litafichua siri na mbinu hizi zinazotumiwa na manguli wakubwa na ambazo sio rahisi kuzipata kwasababu ya gharama yake.
Hivyo nimeamua kuandaa darasa jipya (Kwa lugha ya kiswahili) ambapo utajifunza hatua kwa hatua namna ambavyo mtu yeyote mwenye bidhaa au huduma anaweza akatumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kufulikwa na wateja kama utitiri kwa bajeti ndogo na ndani ya muda mfupi.
Darasa hili nimelipa jina la...
Facebook & Instagram MapeneTM

Kabla sijaongelea kuhusu darasa hiki kiundani zaidi nina ombi moja kwako. Ombi lenyewe ni kwamba...
Tafadhali hakikisha unachokiuza iwe ni bidhaa au huduma ambayo inasaidia kweli wateja kutimiza mahitaji yao maana naogopa nisije nikakupa mbinu hizi adimu halafu ukazitumia kufulikwa na wateja wengi sana kumbe ukawa unawauzia bidhaa au huduma ya hovyo.
Lakini kama una uhakika wa ubora wa bidhaa au huduma yako...
Basi darasa hili ni hatua kwa hatua na fomula iliyokamilika ambayo ipo tayari kwa ajili yako na imekusubiri uifanyie utekelezaji kwenye biashara yako ili uanze kufulika akaunti yako ya Bank kwa Faida za kutosha kwa kufanya matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kwa bajeti ndogo na yanayoleta matokeo ndani ya masaa 72 TU.
Kwa maneno mengine, haijalishi unachokiuza – iwe ni virutubisho lishe, mashuka, mapazia, simu, vifaa vya michezo, vyombo, huduma yoyote n.k fomula hii ya matangazo ya kulipia utakayojifunza kwenye darasa hili itaifanya biashara yako iombe msahama kwa kufulikwa na wateja wengi sana ambao pengine unaweza ukashindwa kuwamudu.
Darasa hili ni taarifa mpya, fursa ya kipekee tofauti na madarasa mengine ambayo ushawahi kuyaona au kuyasikia!
Kwasababu kwenye darasa hili nitakupatia mwongozo A-Z wa kufanya matangazo ya kulipia (Facebook na Instagram) yanayoleta faida kubwa ndani ya mda mfupi (Masaa 72 au chini ya hapo) na kwa bajeti ndogo.
Si hivyo tu...
Nitakusaidia uepuke na usifanye makosa ambayo yanawafanya wafanyabiashara wengi wapoteze pesa, muda na nguvu nyingi bila kupata wateja wengi.
Na zaidi ya yote nitakugeuza kuwa NINJA wa matangazo ya kulipia Facebook na Instagram.
Na hapo bado sijamaliza kuongelea kila kitu utakachokipata kutoka kwenye darasa hili.
Nitakufundisha “Targeting Hack” ambayo ni mbinu pekee inayotumiwa na marketing experts wakubwa Duniani Kama Dan Lok na wengine wengi kugundua makundi ya watu ambao ukiwalenga:
- Unajiondoa kwenye ushindani hivyo kutengeneza faida kubwa ndani ya muda mfupi.
- Kwasababu unakuwa umejiondoa kwenye ushindani, Unamiliki uwanja unapiga pesa za kutosha kwa bajeti ndogo.
Kuna mengi sana ambayo utajifunza kwenye darasa hili, sehemu hii haitoshi kuelezea kila kitu.
Lakini ngoja nikuelezee mambo machache tu kwenye mengi utakayojifunza kwenye darasa hili:
- Namna ya kutumia “Targeting Hack” kugundua “Interests” za watu ambazo ukizilenga unapata Faida kubwa Kwa bajeti ndogo. [ Interests hizi ni ngumu kuzipata kama hujui hii hack. Ukiweza kuitumia hii hack utakuwa umegundua mgodi wa wateja ambao wamekusubiri wakupatie pesa uwauzie bidhaa au huduma yako.
- Hatua 3 MUHIMU ambazo hata mtu ambae hajawahi kufanya matangazo anaweza akazifuata kurusha Tangazo Facebook au Instagram na akawa na uhakika 100% Tangazo hilo litaanza kumpatia matokeo chini ya masaa 72 na kwa bajeti ndogo.
- Kosa 1 la kuepuka kama unataka kupata matokeo ya haraka na faida kubwa kwa kila Tangazo utakalolilipia Facebook au Instagram. [Kibaya ni kwamba 98% wanaofanya matangazo ya kulipia Facebook au instagram wanafanya kosa hili na ndio maana ni ngumu kupata matokeo mazuri]
- Aina 3 za matangazo ambayo yanaleta matokeo ya haraka kwa bajeti ndogo [Moja ya kwanini hupati matokeo mazuri ni uandishi wa Tangazo BOVU lakini baada ya kuzijua aina hizi 3 utakuwa upo kwenye NEEMA ya kufulikwa na wateja]
- Mfano wa matangazo 2 ambayo yashaniingizia Faida ya zaidi ya 15,000,000/=
- Njia 1 ya uhakika wa kujitoa kwenye ushindani ili utumie bajeti ndogo kupata Faida kubwa. (Siku hizi watu wengi sana wanafanya matangazo ya kulipia mtandaoni usipojua kujitofautisha na wao lazima uishie kupoteza hela bila matokeo mazuri]
- Fomula 4 za kuandika “Caption” za kwenye picha ya Tangazo ili mteja ambae yupo tayari kununua ndio asome Tangazo lako. [watangazaji wengi wanaweka captions ambazo zinafanya watu ambao hata sio wateja wasome Tangazo lako hivyo kujikuta unaishia kupata watu wakuulizia bei tu bila kununua]
- Namna ya kutumia application ya Canva kutengeneza picha za mvuto kwa wateja. [Picha nzuri ya Tangazo inafanya watu wakuamini na hivyo kutaka kufanya biashara na wewe]
- Sheria muhimu za kukuongoza kurusha Tangazo Facebook au Instagram. Ukizitii sheria hizi utashangazwa kwa Idadi ya wateja utakaowapata. [Kwa bahati mbaya karibia watu wote wanaotangaza mtandaoni hawazijui sheria hizi kama mwongozo wa kuwa na uhakika wa kupata matokeo mazuri]
- Namna ya kutengeneza mifereji 4 ya wateja wa kudumu Facebook na Instagram [Ukifahamu jinsi ya kutengeneza mifereji hii haitakuja siku itokee uishiwe wateja]
- Ads manager A-Z. Watu wengi hawajui kutumia vipengele vyote vya ads manager ndio maana ni ngumu kupata matokeo mazuri na ya haraka. [Kuna sehemu kadhaa kwenye ads manager ukijua kuzitumia vizuri hutapata shida tena kupata wateja]