Mambo 3 Muhimu Ambayo Kila Networker Anatamani Angeyajua Kabla Hajajiunga Kwenye Biashara Ya Network Marketing!

Mimi ni networker.

Mambo haya 3 ambayo naelekea kukwambia yatawafanya baadhi ya networkers wenzangu wanichukie mpaka mwisho wa dunia.

Lakini kwakuwa kunichukia kwao hakunipunguzii chochote. Lazima ukweli usemwe.

Nafanya hivi kukuonesha kwamba biashara hii ya network marketing ni nzuri sana ila inaharibiwa na sisi tunaoifanya.

Kwa kuyajua mambo haya 3 utaweza kubadili mtazamo wako kuhusu jinsi ya kuifanya biashara hii.

Mambo hayo 3 muhimu ni yafuatayo...

1. Je (Upline wako) aliyekushirikisha biashara hii anajua kuuza?

Najua unatamani sana ungejua kama mtu aliyekushirikisha (Upline wako) anajua au hajui kuuza kabla hujaanza biashara kwasababu kampuni yoyote sahihi ya network marketing ina bidhaa.

Ukiwa kama mwanachama, moja ya njia za kutengeneza hela ni kuuza bidhaa.

Huwezi ukauza bidhaa kama huna ujuzi wa kupata wateja.

Haijalishi bidhaa zina ubora gani lazima awepo mtu wa kuziuza. Hata siku moja bidhaa huwa hazijiuzi zenyewe.

Kwahiyo ifahamike kwamba pesa zipo kwenye kujua kuuza bidhaa na sio kwenye ubora wa bidhaa.

Simaanishi bidhaa zisiwe bora.

Ninachokimaanisha ni kwamba licha ya ubora wa bidhaa lazima awepo mtu mwenye ujuzi wa kupata wateja wa kununua bidhaa vinginevyo bidhaa zitadoda.

Tazama...

Kama aliyekushirikisha biashara hii hana ujuzi wa kupata wateja unategemea baada ya kujiunga kwenye biashara atakufundisha nini?

Kitakachotokea ni kipofu wa kutojua kuuza anamuongoza kipofu mwenzake.

Matokeo yake ndio maana mpaka sasa biashara unaiona ngumu na mwisho wa siku utaacha na kuishia kuisema vibaya biashara hii.

Kwahiyo ni muhimu sana mtu aliyekushirikisha biashara hii awe na ujuzi wa kupata wateja kwasababu baada ya wewe kuanza biashara ni wajibu na jukumu la mtu huyu kukufundisha ujuzi huo ili na wewe uuze bidhaa ndio utengeneze hela.

Kama hajui kazi unayo tena sio ya kitoto.

Na ikumbukwe kampuni haikulipi hela kwa kuwa mwanachama. Inakulipa pale ambapo unakuwa umefanya mauzo ya bidhaa au umeingiza mtu kwenye fursa.

Ukishindwa kuuza kosa halipo kwenye kampuni. Kosa lipo kwa aliyekushirikisha kushindwa kukufundisha kuuza.

Kwahiyo kama nyote hamjui kuuza inatakiwa uweke jitihada binafsi za kujikomboa vinginevyo utaishia kuwa msindikizaji.

Tuendelee na jambo la...

2. Je aliyekushirikisha biashara hii ana uwezo kweli wa kukufundisha na wewe ukajua kuuza?

Nisikilize kwa makini...


Kujua kuuza na kuwa na uwezo wa kumfundisha mtu kujua kuuza kama wewe unavyofanya ni mambo 2 tofauti kabisa.


Kuna mtu anaweza akawa anajua kuuza lakini asiwe na uwezo wa kukufundisha vile anavyofanya kupata wateja.


Na kuna mtu anaweza akawa anajua kuuza na pia akawa na uwezo wa kukufundisha wewe kupata wateja kama yeye anavyofanya.


Kwahiyo licha ya mtu aliyekushirikisha biashara hii kutakiwa kujua kuuza inabidi awe pia na uwezo wa kukufundisha wewe vile anavyofanya kupata wateja.


Kuna maana gani yeye kujua kuuza halafu asijue kukufundisha vile anavyofanya? Maana yake ukijiunga kwake imekula kwako lazima usote kupata wateja.


Kwahiyo kama hajui naelewa ni kwa kiasi gani unatamani ungejua kabla hujajiunga kwake lakini ndio hivyo imeshatokea.


Kazana ujikomboe kabla hujachelewa.


Tumalizie jambo la...

3. Je aliyekushirikisha biashara hii alikuwa tayari kukudhihirishia kwamba jambo la kwanza na la pili anaviweza kweli kabla ya wewe kuanza biashara rasmi?

Ndio aliyekushirikisha biashara hii anaweza akawa kweli anajua mbinu za kupata wateja na pia akawa na uwezo wa kukufundisha na wewe kufanya vile anavyofanya lakini...


Utajuaje? Au Utaaminije?


Maneno matupu hayavunji mfupa.


Na networkers tulio wengi tuna maneno ya ushawishi wa kumshawishi mtu kwamba akianza biashara tutamsapoti lakini mwisho wa siku ukianza biashara tunakuacha solemba.


Kwahiyo kama aliyekushirikisha biashara hii alikwambia ukianza biashara ndio atakufundisha mbinu za kuuza nadhani mpaka sasa ushagundua Mtu huyo hajui kuuza au anajua.


Kama anajua hongera sana. Shikamana nae mpambanie ndoto zenu.


Lakini taarifa mbaya ni kwamba ni wachache sana wanaojua kuuza na wakakufundisha vile wanavyofanya.


Kwahiyo nina uhakika utakuwa miongoni mwa watu wengi ambao wanaendelea kuhangaika.


Nadhani unatamani sana ungejua kama aliyekushirikisha biashara hii hajui kuuza ili usijiunge kwenye timu yake. Si ndio?


Tunarudi tena kwenye swali letu. Ungejuaje sasa kama anajua kuuza na anauwezo wa kukufundisha na wewe ukajua kuuza?


Jibu lipo moja tu.


Ilitakiwa mtu huyo ambae alikushirikisha kabla ya wewe kuanza biashara akudhihirishie kwa kukufundisha kupata wateja.


Ukipata wateja kabla hujaanza biashara nadhani ni ishara tosha kwamba ukianza biashara utafanikiwa.


Mambo hayo 3 ndio msingi wa mafanikio kwenye biashara hii. Bila mambo hayo 3 huwezi ukafanikiwa hata siku moja kwenye biashara hii.


Networkers wengi najua wanatamani sana wangeyafahamu mambo hayo 3 kabla ya kuanza biashara hii ya network marketing...


Kwasababu utagundua sapoti uliyoahidiwa kabla hujaanza biashara haipo zaidi ya kuhimizwa kuhudhuria mikutano na mafundisho yasiyo changia kuongeza mauzo au kukuza timu yako.


Lakini imeshatokea.


Sasa ufanye nini?


Nisikilize kwa makini...


Kuuza na kuingiza watu kwenye fursa ndio njia 2 pekee kwenye biashara hii ambazo zitakuingizia kipato.


Tofauti na hapo utajikuta tu wewe ni msindikizaji.


Lakini usijali nataka (Kama utaniruhusu) nikufundishe hatua 2 za kupata wateja kwa kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni.


Kwa maelezo zaidi kuhusu hatua hizi 2 bonyeza hapa chini sehemu iliyoandikwa "Naomba Maelezo Zaidi"


Cheers,

Mr Bokko.

This site is not a part of the FacebookTM website or FacebookTM  Inc. Additinally, this site is NOT endorsed by FacebookTM  in any way. FACEBOOKTM is a trademark of FACEBOOKTM, inc.  

Copyright - Online Marketing System Pro

>
error: Copying is not allowed on this website
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications