Kama matangazo yako ya Meta yanakupatia wateja lakini kila ukijaribu kuongeza bajeti unaishia kuchoma hela – umefika mahali sahihi...

HATIMAYE IMEVUJISHWA: Siri Ya Andromeda Ambayo Itakuonesha Hatua Moja Unayokosea Ili Matangazo Yako Yateme MAFULIKO YA WATEJA Bila Kuchoma Bajeti.

Angalia video hii kabla hujaongeza tena bajeti yako ukatonesha kidonda cha kuchoma bajeti kubwa bila kupata wateja wengi

Kutoka kwa: Mr Bokko

Godfather wa Meta Ads Tanzania.

Dar es Salaam.


Mabadiliko ya mfumo wa matangazo ya kulipia Meta (Facebook & Instagram) yameibua matabaka matatu ya wafanyabiashara.

  1. Wafanyabiashara ambao bado wanacheza mchezo wa zamani. Ambao zama zake zimeshapita.

Hawa ni wale ambao bado wanarusha matangazo yao kizamani bila kutambua wanajenga uadui na mfumo mpya wa matangazo ya kulipia wa Meta unaoitwa: Andromeda

Ukweli mchungu ni kwamba Andromeda inawachukia sana wafanyabiashara ambao bado wanarusha matangazo kizamani…

Kwa sababu wanakinzana nayo. Yenyewe inataka mchezo uchezwe na ngoma za kisasa zaidi lakini wao wanacheza mchezo kwa ngoma ambazo ni zilipendwa.

Kwahiyo sasa, ukirusha matangazo kizamani maana yake unaiambia Andromeda ifanye kazi ambayo ilikuwa inafanywa na mfumo wa zamani. Kitu ambacho hakiwezekani.

Matokeo yake ni kwamba wanaishia kuchoma bajeti kila siku na kuona matangazo ya kulipia hamna kitu.

Lakini kuna kina hawa hapa…

    2. Wafanyabiashara ambao wanacheza mchezo wa matangazo ya kulipia kisasa zaidi.

Hawa wanaelewa kwamba zama zimebadilika. Mfumo wa matangazo ya kulipia wa zamani sio wa sasa.

Wa zamani ulichezwa kivyake. Na huu wa sasa unachezwa kwa style yake mpya.

Na wanaocheza mchezo huu kisasa, Andromeda INAWAZAWADIA MAFULIKO YA WATEJA.

Na wakati wanaocheza kwa njia za kizamani, Andromeda inaumia kuona bajeti zinalika tu bila matokeo mazuri.

Swali kwako: Unacheza mchezo mpya wa Andromeda kama inavyokutaka ucheze au bado unacheza kizamani?

Baada ya kuangalia video ya sehemu ya kwanza ya kozi yangu mpya inayoitwa “Meta Ads Mastery” hapo juu jibu unalo.

Na ni wazi kwamba Meta Ads Mastery ni daraja la kukutoa kwenye kundi la kwanza la wafanyabiashara kwenda kwenye kundi la pili.

Aidha upite darajani uvuke salama au ujaribu kuruka mto mkubwa bila kupita darajani uishie kuelea majini.

Tayari nimeshakutengenezea daraja…

Je, uko tayari kulitumia?

Tazama, sihitaji nikushawishi sana kujiunga kwenye kozi ya Meta Ads Mastery….

Kwa sababu naamini video hiyo hapo juu ambayo ni sehemu ya kwanza kati ya sehemu tano za kozi hii mpya, inatosha kukufanya uone uzito na thamani ya kilichopo mbele yako.

Ukweli ni kwamba “Meta Ads Mastery” ni dhahabu ambayo iko sehemu ya wazi kabisa mbele yako.

Uamuzi ni wako. Uichukue ukabadilishe maisha ya biashara yako au ufanye kama vile hujaiona umuachie mfanyabiashara mwenye njaa kali ya kukuza biashara yake aanze kupata MAFULIKO YA WATEJA — uanze kumuona ni mchawi.

Hata hivyo, haya hapa ni baadhi ya mambo machache kati ya mengi ambayo utajifunza kutoka kwenye sehemu nne zilizobaki za Meta Ads Mastery.

Part 1: Understanding The Algorithm

Kuelewa jinsi mfumo mpya wa matangazo ya kulipia Facebook & Instagram (Andromeda) unavyofanya kazi na unakutaka wewe mrusha matangazo ufanye nini kupata matokeo mazuri.

Hii sehemu tayari umeangalia kwenye video hapo juu. Kama hujaangalia video hiyo, hakikisha unaangalia mwanzo mpaka mwisho.

Hata hivyo, itakuwepo ndani ya kozi kwa ajili ya marudio maana yaliyomo ni “heavy” kiasi cha kwamba kuangalia mara moja tu haitoshi.

Part 2: Creative Research & Production

Baada ya kuelewa jinsi Algorithm mpya inavyofanya kazi, sasa utajifunza kutumia mfumo wangu wa Avatar Discovery System kuitengenezea Andromeda risasi (creatives) zinazolenga walengwa sahihi.

Part 3: Campaign Structure & Testing

Baada ya kutengeneza risasi hizo, utajifunza mfumo mpya wa kupangilia matangazo na jinsi ya kubaini ni tangazo lipi hasa linalokuletea MAFULIKO YA WATEJA

Part 4: Scaling Winners

Baada ya kubaini tangazo linalokuletea MAFULIKO YA WATEJA, sasa ni wakati wa kulifanya LISABABISHE MAFULIKO ENDELEVU YA WATEJA bila kuharibu performance yake.

Part 5: Launching Ads

Tunamalizia kwa kutekeleza kila kitu ulichojifunza kuanzia Part 1 mpaka Part 4 kwa vitendo ndani ya Ads Manager, hatua kwa hatua, mpaka uweze kurusha campaigns zako kwa usahihi.

Mpaka sasa najua unajiuliza swali moja tu kichwani mwako…

Meta Ads Mastery Inagharimu Kiasi Gani?

Fikiria hili…

Nimewekeza  dola 2997 (Tsh 7,000,000+) kupata haya madini yaliyomo kwenye Meta Ads Mastery. 

Lakini wewe utalipia Tsh 150,000 tu kuyapata. 

Niambie kama huo sio wizi ni nini.

Ni sawa na kusema nipe Tsh 150,000 halafu mimi nikupe Tsh 7,000,000 

Hata hivyo, kama utakuwa miongoni mwa watu 100 wa kwanza, utajipatia kozi hii kwa bei sawa na jeans moja pale kariakoo.

Tsh 45,000 Tu

(Una-save  Tsh 105,000 nzima)

Chaguo ni lako, aidha ukanunue jeans moja kariakoo kwa Tsh 45,000 ambalo ndani ya mwezi litakuwa limeshaanza kupauka na unafikiria kununua lingine…

Au ulipie Meta Ads Mastery kwa Tsh 45,000 ikuletee MAFULIKO YA WATEJA kwenye biashara yako na utengeneze faida kubwa ya kuweza kununua jeans hata 100 huku biashara yako ikiendelea kufurahia MAFULIKO HAYO YA WATEJA.

Lakini inabidi ufanye maamuzi haraka kwa sababu wakitimia watu 100 wa kwanza, bei inarudi kwenye Tsh 150,000.

Wafanyabiashara watakao jiunga kwenye kozi hii leo, ndani ya siku 30 zijazo watakuwa kwenye maandalizi ya KUPOKEA MAFULIKO YA WATEJA kwenye biashara zao. 

Swali pekee kwako ni hili: Je, utaungana nao mnufaike pamoja au utawaangalia wanufaike wao peke yao huku biashara yako ikiendelea kugeuka kuwa JANGWA la kukosa wateja?

Naelewa.

Kuna watu ambao wanasema...

"Mr Bokko mimi ningependa unifanyie tu mwenyewe hayo matangazo kwa sababu niko bize sana sitoweza kufuatilia darasa mwanzo mpaka mwisho au mtaalamu wangu anayenirushia matangazo kwa sasa hayaniletei matokeo mazuri"

Kama huyo ni wewe – basi upo kwenye kundi hili...

      3. Wafanyabiashara wanaotaka kurushiwa au wanaorushiwa tayari matangazo yao na wataalamu wanaocheza mchezo wa zamani.

Hili ni kundi la wafanyabiashara ambao jukumu la kurusha matangazo ya kulipia wameliweka mikononi mwa watalaamu ambao bado wanacheza mchezo mpya kwa njia za kizamani.

Matokeo yake unaishia kuchoma bajeti yako na ukiwauliza nini kinaendelea wanakwambia ili upate matokeo mazuri unatakiwa uongeze bajeti, kitu ambacho kinafanya hali kuwa mbaya zaidi.

Nini ufanye sasa?

Chaguo ni lako…

Aidha wao wabadilike wajifunze kucheza mchezo huu kisasa zaidi ili wakupatie matokeo unayotaka au…

Wewe umkabidhi jukumu hilo mtaalamu mwingine ambaye tayari anajua kucheza mchezo kisasa zaidi.

Kumbuka biashara yako inahitaji wateja tangu jana.

Kumsubiri mtaalamu wako wa sasa mpaka ajifunze kucheza mchezo kisasa zaidi ni sawa na kufunga biashara yako kwa muda.

Je, upo tayari kuvumilia hizo siku ambazo mtaalamu wako atakuwa anajifunza kucheza mchezo mpya na kuanza kufanya majaribio kwenye biashara yako?

Jibu liko wazi.

Kwanini usinitumie mimi ambaye tayari nauelewa mchezo mpya nje ndani na nipo tayari kuanza kuipa biashara yako pumzi ya wateja hata kuanzia leo?

Hata hivyo, sitoi huduma hii ya kusimamia kurusha matangazo kwa kila mtu.

Lazima ukidhi vigezo vyangu.

Vigezo vyenyewe ni hivi hapa.

  1. Lazima uwe na bajeti ya kurusha matangazo isiyopungua Tsh 1,000,000
  2. Lazima uwe tayari kufuata kile nitakachokuelekeza ufanye na sio wewe tena kunielekeza mimi nifanye nini.

Kitu cha mwisho ambacho sitaki kukiona ni mfanyabiashara kunilipa pesa nisimamie matangazo yake ya kulipia halafu aanze kunielekeza nini nifanye kulingana na vitu anavyojifunza kutoka kwa watu wengine.

Kama huyo ni wewe, samahani sana. Hatuwezi fanya kazi pamoja.

Nishavuka hiyo level ya ku-deal na watu wasumbufu kwa sababu ya pesa.

Simaanishi nina hela nyingi. Pointi yangu ni kwamba maisha ni mafupi sana kutumikia pesa inayokufanya uishi kwa kuteseka kufanya unachokifanya.

Kwahiyo kama hukidhi vigezo hivyo viwili, basi huduma yangu ya kusimamia biashara yako katika upande wa matangazo ya kulipia sio kwa ajili yako.

Lakini kama unakidhi vigezo hivyo, huduma hii inajumuisha yafuatayo:

  • Kutafutiwa avatars—makundi yaliyojificha ndani ya soko lako. Makundi haya ndio msingi wa kutengeneza matangazo yenye kuleta MAFULIKO YA WATEJA.
  • Kutengenezewa matangazo ambayo Andromeda inahitaji ili kukupa MAFULIKO YA WATEJA.
  • Kurushiwa hayo matangazo na kuhakikisha biashara yako INAFULIKWA NA WATEJA.
  • Kusimamia hayo matangazo kwa MWEZI MZIMA kuhakikisha MAFULIKO YA WATEJA HAYAKOMI
  • Ikitokea matangazo yakaanza kutoleta MAFULIKO YA WATEJA, nakutengenezea mengine mapya na kuhakikisha MAFULIKO YA WATEJA yanaanza upya.
  • Kiufupi nasimamia jukumu zima la matangazo ya kulipia. Kazi yako ni moja tu: KUPOKEA MAFULIKO YA WATEJA.

Najua kwa sasa unajiuliza swali moja kichwani mwako:

Gharama Za Usimamizi Wa Matangazo Ya Kulipia Zipoje?

Uzito wa kazi hii unaujua.

Ingekuwa rahisi ungejifanyia mwenyewe.

Na wala usingekuwa unasoma mpaka hapa ulipofikia.

Ungekuwa bize unajirushia matangazo mwenyewe.

Lakini bado unaendelea kusoma.

Ebu fikiria hili…

Unampa mtu bajeti ya Tsh 1,000,000 halafu lengo lako ahakikishe inaleta wateja wa kukupatia faida mara 2,3 au hata mara 4 ya hela uliyowekeza kwenye matangazo….

Huyo mtu upo tayari kumlipa shingapi?

Ukimlipa kidogo, huo unakua ni unyonyaji.

Wewe upate zaidi halafu yeye umlipe kidogo. Kweli?

Sio kweli. Si ndiyo?

Basi utapata huduma ya usimamizi wa matangazo ya kulipia kwa bei ya kizalendo kabisa ya…

Tsh 350,000 Tu

Tsh 350,000 ni gharama ya usimamizi wa mwezi mmoja. Kama utaendelea kufanya kazi na mimi tutaambiana gharama mpya kulingana na ukubwa wa biashara yako.

Lakini pia, kwa Tsh 350,000 inakuwa ni usimamizi wa matangazo ya bidhaa moja. Kama utahitaji nisimamie matangazo ya bidhaa zaidi ya moja gharama yake ni tofauti na hiyo.

Kwa wewe ambaye hukidhi vigezo vya huduma hii au Tsh 350,000 kwako ni kubwa kwa sasa…

Sijakusahau.

Unaweza kujiunga kwenye kozi ya Meta Ads Mastery ili ujifunze kujirushia matangazo mwenyewe.

Bei yake ni Tsh 150,000

Lakini ukiwa miongoni mwa watu 100 wa kwanza, utalipia…

Tsh 45,000 Tu

(Una-save  Tsh 105,000 nzima)

Tukutane darasani.

Ni mimi Godfather wa Meta Ads,

Mr Bokko.

>
error: Copying is not allowed on this website
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications