• Home
  • |
  • Blog
  • |
  • Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

August 22, 2022

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Kati ya kuuza Bidhaa na kuingiza watu kwenye fursa Kipi unadhani kitakupatia uhuru wa kipato?

Jibu liko wazi.

Lakin kabla sijatoa jibu la Swali Hilo, Kuna kitu ningependa Utambue.

Kitu hicho ni kipi Mr Bokko? Kitu hicho ni hiki...

Kuna Njia kuu 2 tu za kutengeneza pesa kwenye kampuni yoyote ile ya Network marketing.

Ndio, unaweza ukatengeneza pesa Kwa njia zaidi ya hizi 2 lakini njia Hizi 2 ndo baba na mama wa njia zingine zote.

Njia Hizi ni zipi sasa?

Una Haraka kwel kama mtoto mdogo aliyeambiwa badae atapelekwa dukani kuchagua nguo. Utakuta Kila muda mama tunaenda sangapi?

Ohoo nisamehe bure maana nimeshaanza tantalinta nyingi.

Haya Hizi hapa njia kuu 2 za kutengeneza pesa kwenye kampuni yoyote ile ya Network marketing...

1. Kuingiza watu Kwenye fursa ya biashara (recruiting/ sponsoring)

2. Kuuza Bidhaa kwa rejareja (retailing)

Tuanze na...

1. Kuingiza watu Kwenye fursa yako ya Biashara!

Sina kipya Cha kuelezea Hapa Maana kama unafanya biashara ya Network marketing nadhani unaelewa kuhusu kuingiza watu Kwenye fursa labda usichokielewa ni mbibu za kupata watu wakuwaingiza.

Kwa bahati MBAYA somo hili la leo halihusu mbinu na namna ya kuingiza watu Kwenye fursa.

Ok. tuachane na hayo.

Ninachotaka kuzungumzia kuhusu njia Hii ni hiki...

Kupitia njia Hii ya kuingiza watu Kwenye fursa ndo tunapata neno Network yaani mtandao WA watu

Maana yake Nini?

Maana yake ni kwamba...

Hii ni biashara ya kutengeneza mtandao wa watu ambapo nyote Kwa pamoja mtazidi kukuza mtandao huo na kuuza Bidhaa

Ebu Rudia kusoma maneno hayo hapo juu!

Umeyaelewa maneno hayo?

Maana yake rahisi ni kwamba...

Biashara hii sio sawa na ajira na wala sio biashara ya kufanya wewe mwenyewe.

Chochote utakachokifanya inatakiwa Hata wengine ambao wapo kwenye mtandao wako wakifanye pia.

Ukikomaa kukifanya mwenyewe Maana yake umejipa kazi na ajira ambayo hakuna mwajiri wake.

Kwahiyo Kiufupi, njia Hii ya kwanza ndo inayoleta maana halisi ya network marketing

Kama kampuni uliyopo hakuna kuingiza watu basi tambua kwamba hiyo Sio network marketing Bali ni scam.

Sasa kama hakuna kuingiza watu hiyo network inatoka wapi?

Ogopa sana makampuni wanayosema huhitaji kuingiza watu sisi ni kuuza tu.

Kama kampuni yako ni ya hivyo kimbia mapema sana.

Umenielewa rafiki yangu? Eeeh kimbia.

Sasa...

Iko hivi…

Kupitia kuingiza watu Kwenye fursa utalipwa Hela au commission au vyovyote vile kulingana na utaratibu Wa kampuni uliyopo.

Utakavyozidi kuingiza watu Maana yake utatengeneza mtandao mkubwa wa Watu chini yako.

Watu Hawa wakifanya kazi utalipwa. Wasipofanya kazi hulipwi ni sawa na kazi BURE.

Kwahiyo ubora wa Watu unaowaingiza ndo kitu Cha msingi sana na Sio wingi wa Watu unaowaingiza.

Maana yake Nini?

Maana yake ni kwamba....

Kama una mashine za Kazi chini yako upo kwenye neema na utalawa wa kampuni uliyopo.

Hata siku ukiamua kulala mwezi mzima Ukiwa unakoroma kitandani ukiamka tu na kuchungulia kwenye account yako unakuta pesa zimerundikana kama mafungu ya yanya.

Unapiga miayo kidogo halafu unasema Ngoja niende zangu lunch Verde Zanzibar.

Kwanini?

Kwasababu una mashine za Kazi chini.

Ni pesa inaingia tu ufanye kazi au usifanye kazi.

Huo ndo uhuru wa kipato ambao tunauzungumzia.

Sio mpaka kazi ufanye wewe kama ajira ndo upate Hela.

Tazama, huu ndio upekee wa biashara ya Network marketing kwa biashara zingine.

Vipi ukiamua ukorome kitandani Kwa mwezi mzima bila kufanya chochote halafu huna mashine za kazi chini yako?

Jibu nadhan unalijua. Meno yatatoa harufu halafu hata Hela ya kununulia dawa ya meno huna. Aisee!

Inatosha. Tuendelee na njia ya pili.

2. Kuuza bidhaa Kwa rejareja!

90% ya networkers wanachokifanya ni hiki.

Simaanishi ni kitu kibaya. Hapana.

Ni kitu kizuri.

Lakini... (Nitakwambia hapo mbele kidogo)

Kwa mfano:

Ukipata mgojwa wa kisukari ukamuuzia virutubisho lishe unakuwa umefanya mauzo ya rejareja.

Kiufupi ukimuuzia mteja yeyote virutubisho lishe vya kumsaidia kuondokana na tatizo lake la kiafya unakuwa umefanya mauzo ya rejareja.

Sasa...

Ni 10% tu ya networkers wote ambao nguvu Yao kubwa ipo kwenye njia ya kwanza ya kutengeneza pesa na 90% (hata wewe upo kwenye kundi hili) nguvu Yao yote wameielekezea kwenye kuuza bidhaa.

Sasa tazama...

Unadhani Kati ya makundi haya 2 ya wanaoingiza watu Kwenye fursa Sana na wanaouza Sana lipi ni kundi lipo kwenye neema ya uhuru wa kipato?

Wanaouza Sana? Pole kama unawaza hivyo.

Kuuza sana hakuleti maana halisi ya Network (mtandao wa watu)

Kama unauza Sana hongera sana Maana huwezi kulala njaa na Wala huwezi kushindwa kulipa Kodi ila Hela hiyo haitakufanya ununue “the queen of the Road, a.k.a Rolls Royce”

Kama hujui rolls Royce ni Nini nenda ukagoogle.

Au Hela ya kuuza Sana haitakufanya ujenge ghorofa. Sahau Hilo.

Rafiki yangu, kuuza Sana hakutokufanya ununue Bugatt Wala Range, Wala Ferrari, Wala yatch Wala private jet Wala kitu chochote Cha gharama kubwa Sana.

Kuuza sana kutakutimizia Mahitaji yako madogo na sio ndoto zako kubwa.

Labda nikuulize swali...

Unadhani wanaotengeneza Hela nyingi Kwenye kampuni uliyopo wanauza sanaaaa?

Hapana Hata hawauzi sana. Wapo kwenye asilimia 10 ya watu wanaoingiza watu wengi kwenye fursa na Kutumia nguvu kazi ya wengine kujitengenezea kipato.

Endelea kuuza Sana Maana ni Jambo zuri lakini kama Unataka mambo mazuri ya dunia ya Mungu wetu mwema huyapati Kwa kuuza Sana ndugu. I'm sorry!

I really am.

Eti nimeongea kiingereza Sasa. Wakati ukiniambia tukiongee wiki nzima nakimbia mbio!

Anyway, ngoja nikutolee mfano mmoja...

Mfano:

Kuna Watu 2. Mtu A na mtu B.

Mtu A ana mashine za Kazi 10 chini yake. Yaani ana watu 10 wachapa kazi kwenye mtandao wake.

Watu Hawa kawaingiza kwenye biashara kupitia njia ya kwanza ya (recruiting/sponsoring)

Na mtu B Hana mashine za Kazi hata moja chini yake.

Lakin MTU B anajua kuuza Sana.

Mtu A ni mashine ya kazi Maana asingepata mashine za Kazi 10 kizembe.

Sasa tuone ni yupi atatengeneza Hela Sana kuliko mwingine.

Tazama...

Mtu A akifanya kazi yoyote iwe kuingiza watu au kuuza atalipwa. Lakini kwakua ana mashine za Kazi chini yake atalipwa zaidi kupitia kile ambacho mashine za Kazi Zitakua simekifanya.

Na Cha zaidi ni kwamba Hata akiwa anaumwa mashine zake za Kazi zikafanya kazi atazidi kutengeneza pesa.

Kwahiyo mtu A afanye kazi asifanye kazi mpunga lazima apate kama kawaida.

Sasa tuone mtu B.

Mtu B anauza Sana. Yani Sana.

Anatengeneza pesa kweli. Lakini siku akiacha kuuza au akaugua ndo habari ya kutengeneza pesa imeishia hapo.

Kwahiyo Ili mtu B atengeneze pesa itambidi afanye kazi Kila siku kama mtumwa vinginevyo hana chake.

Kwahiyo Sasa...

Tukirudi kwenye swali letu...

Kati ya kuingiza watu Kwenye fursa yako ya Biashara ya Network marketing na kuuza kipi kitakupatia uhuru ya kipato?

Jibu sahihi: Kuingiza watu Kwenye fursa ya biashara yako kutakupatia uhuru wa kipato.

Naomba nieleweke vizuri.

Sijasema kuuza ni vibaya. Kama upo makini nimesema ni kuzuri lakini kuuza Sana kutakusaidia kutimiza Mahitaji madogo madogo na sio kutimiza ndoto zako kubwa.

Kwa Leo niishie hapo.

Ni mimi, Rafiki yako kipenzi,

Mr Bokko!

P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.

P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.

Related Posts

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Mr Bokko


Mr Bokko ni Social Media Marketing & Advertising Expert + Founder & CEO wa Online Marketing System Pro Co Ltd - Kampuni yenye kuwasaidia Wafanyabiashara na Wajasiriamali njia rahisi ya kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni (Facebook & Instagram) kuweza kunasa wateja pasipo kupoteza muda na pesa kwenye njia ambazo hazifanyi kazi.

Your Signature

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}
>
error: Content is protected !!
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications