• Home
  • |
  • Blog
  • |
  • Hatua 3 Pekee Za Kupata Prospects Ambao Wapo Tayari Kujiunga Kwenye Timu Yako!

August 21, 2022

Hatua 3 Pekee Za Kupata Prospects Ambao Wapo Tayari Kujiunga Kwenye Timu Yako!

Je na wewe unaamini kukosa prospects wa kujiunga kwenye timu yako ni tatizo kama wengi wanavyodhania?

Sio kweli.

Kukosa prospects wa kujiunga kwenye timu yako sio tatizo hata siku moja.

Bali ni dalili ya tatizo.

Ni kiashiria tu cha kuonesha kwamba kuna tatizo.

Ndio ni kweli prospects ni mafuta ya kuchochea gurudumu la biashara yako isonge mbele.

Lakini unaweza ukapewa prospects wote duniani na bado usiweze kuingiza kwenye fursa yako hata mmoja wao.

Ndio maana ukosefu wa prospects wa kutosha wa kujiunga kwenye biashara yako sio tatizo.

Tatizo ni nini sasa?

Tatizo ni wewe mwenyewe.

Ndio, wewe mwenyewe.

Kwasababu ya uchoyo na ubinafsi wako.

Wewe ni mchoyo na mbinafsi kwasababu haiwezekani umwambie prospect kwamba ajiunge kwanza halafu ndio utamfundisha namna ya kuifanya biashara hii ya network marketing.

Kwanini usimfundishe kwanza halafu ndio umwambie ajiunge kwenye team yako?

Hata kama ni mimi huwezi ukaniambia jiunge kwanza halafu mafunzo ndo yatafuata baada.

Kuna utofauti gani na kumwambia mteja “Nunua kwanza halafu baada ya kununua nitakuelezea kazi ya dawa hii”

Ungekuwa wewe ungenunua? Wala usingenunua.

Kwahiyo kukosa prospects wa kutosha ni dalili ya kuonesha kwamba wewe ni mchoyo na mbinafsi.

Unachokijali ni prospects wajiunge utengeneze zako hela kwisha habari.

Lakini unadhani nani atajali endapo wewe hujali?

Kumbuka hakuna mtu anataka unachokitaka wewe.

Kila mtu anataka anachokitaka yeye.

Kwahiyo itakuwa ngumu kuipata pesa ya mtu aliyoipata kwa mbinde na shida endapo hutojali anachokitaka yeye.

Na kibaya zaidi unawauzia prospects wako fursa ambayo sio kitu wanachotaka kununua.

Kumbuka wewe ndio bidhaa ya biashara yako.

Ukiwa kama bidhaa ya biashara yako, wewe ni bora kiasi gani kumfanya prospect atake kukununua?

Haishangazi kwanini huna team kubwa kwasababu huna ubora wowote wa kumfanya prospect atake kukununua (kujiunga kwenye team yako)

Ndio maana mara nyingi prospects huwa wanakimbilia kujiunga kwa viongozi wakubwa ambao wameshatengeneza hela nyingi.

Kwasababu tu viongozi ambao wameshatengeneza hela nyingi ni bidhaa bora za kununuliwa.

Usinielewe vibaya.

Simanishi kuwa na hela nyingi ndo kuwa bidhaa bora. Hapana.

Ila kuwa na hela kunakufanya uonekane wewe kuwa na utofauti na wengine kwahiyo hali hiyo itawafanya prospects watake na wao uwafundishe siri ya mafanikio yako ndio maana watakukimbilia uwaunge kwenye fursa yako.

Sasa kama hujawahi kutengeneza hela nyingi ufanyeje ili prospects wajilete wao wenyewe kwako?

Rahisi sana.

Fata hatua 3 zifuatazo:

Hatua ya kwanza:

Tafuta mentor ambaye anatumia njia ya kipekee zaidi kuifanya biashara hii ya network marketing ujifunze kutoka kwake.

Siku zote siri ya mafanikio ni kutafuta mtu ambaye kafanikisha kupata kile unachokitaka ili ufanye kama yeye alivyofanya kukipata.

Kwahiyo jifunze kwa walio kutangulia.

Kwa mfano mimi nilijua mpaka biashara ya network marketing inafika Africa lazima Nchi za wenzetu kwa mfano Marekani wapo wengi sana ambao wameshapata mafanikio makubwa.

Kwahiyo nilichokifanya ni kutafuta mentors ambao walitumia njia ya kipekee zaidi kupata mafanikio makubwa ili nami wanifundishe njia hiyo niitumie kufikia malengo yangu.

Na kwa sasa njia hiyo niliyofushishwa na manguli wa manguli ndio ninayoitumia mimi na team yangu.

Hivyo basi na wewe tafuta mentors wa kukuambukiza kile wanachokijua na walichokifanya kupata unachotamani na wewe kupata.

Tukiendelea na...

Hatua ya pili:

Chagua aina ya prospects ambao unatamani ufanye nao kazi pamoja kwenye team yako.

Achana na habari za kutaka kila mtu ajiunge kwenye team yako.

Kwasababu unatakiwa uelewe kwamba...

Kila mtu ni prospect lakini prospect wako wewe sio kila mtu

Kwahiyo yakupasa uchague aina ya watu ambao unawataka kwenye team yako halafu baada ya hapo utumie mluzi kuwaita huko mtandaoni.

Kwa mfano: Kama unahitaji kuongea na Juma lakini Juma yupo kwenye chumba ambacho kimejaa watu wengi unachokifanya kumpata juma ni kipi?

Unaanza kumtafuta alipo?

Huo ni upotezaji wa muda.

Na utatumia nguvu nyingi.

Njia rahisi ya kumpata juma ni kuita jina lake.

Baada ya kuita jina lake mhusika atakufata mwenyewe.

Unaona? Nguvu kidogo na kazi kidogo unampata mhusika.

Kwahiyo ndio maana inatakiwa uamue ni prospects wa aina ipi unataka uwe nao kwenye team yako ili sasa huko mtandaoni ukatumie lugha ambayo prospects hao tu watatambua kwamba unazungumza nao moja kwa moja.

Tumemaliza?

Bado. Una haraka ya kwenda wapi.

Ngoja nimalizie...

Hatua ya tatu:

Anza kuifundisha njia hiyo ya pekee uliyofundishwa na Mentors wako kwa prospects wako kabla hata hujawambia habari za kujiunga kwenye team yako.

Prospects wako watajuaje kama unajua kweli pasipo wewe kuwafundisha kwanza?

Lazima uwape kionjo cha kile ulichofundishwa na mentors wako ili kuwatamanisha na kuwafanya wakung’ang’anie uwafundishe zaidi na zaidi.

Toa elimu ya bure kwanza kwa prospects wako kwasababu kwa kufanya hivyo utaonekana kuwa bidhaa bora ambayo mtu atatamani afanye nayo kazi pamoja.

Na huo ndio mwisho wa hatua 3 za kupara prospects ambao wapo tayari kujiunga kwenye timu yako.

Cheers,

Mr Bokko.

P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.

P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.

Related Posts

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Mr Bokko


Mr Bokko ni Social Media Marketing & Advertising Expert + Founder & CEO wa Online Marketing System Pro Co Ltd - Kampuni yenye kuwasaidia Wafanyabiashara na Wajasiriamali njia rahisi ya kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni (Facebook & Instagram) kuweza kunasa wateja pasipo kupoteza muda na pesa kwenye njia ambazo hazifanyi kazi.

Your Signature

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}
>
error: Content is protected !!
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications