• Home
  • |
  • Blog
  • |
  • Haya Hapa Makundi 2 Ya Watu Sahihi Ambao Wapo Tayari Uwashirikishe Fursa Yako!

August 19, 2022

Haya Hapa Makundi 2 Ya Watu Sahihi Ambao Wapo Tayari Uwashirikishe Fursa Yako!

Umeshawahi (Hata kwenye TV) kumuona simba akiwa mawindoni?

Ona ukielewa vizuri anachokifanya utaweza kujenga timu kubwa sana ndani ya muda mfupi.

Ngoja tuone anachokifanya...

Simba akiwa mawindoni huwa hakurupuki kuanza kumkimbiza mnyama yeyote.

Anachokifanya ni...

Anatishia kundi la wanyama wengi ili abaini ni kamnyama gani hakawezi kukimbia vizuri ale nako sahani moja.

Akishakajua kamnyama ambako hakajiwezi anakakimbiza hako hako masikini hadi anakala nyama.

Tazama...

Simba anajua licha ya kuwa na mbio kali lakini kuna baadhi ya wanyama wanatimuka mbio zaidi yake.

Kwahiyo akiwakomalia wanyama wenye mbio kali zaidi yake atakufa njaa siku zote.

Stori hii ina uhusiano gani na kujenga timu kubwa?

Iko hivi...

Networkers wengi wanapata shida na kuhangaika kupata watu wakujiunga kwenye fursa kwasababu unadhania kila mtu ataipenda na kutaka kujiunga kwenye fursa yako.

Sio kweli.

Fursa yako sio kwa ajili ya kila mtu.

Usije ukadanganywa hata siku moja kwamba kila mtu ataipenda fursa yako.

Haijalishi ubora wa bidhaa au uzuri wa mfumo wa malipo.

Bado kuna watu wengi hawataipenda fursa yako.

Kwahiyo unachotakiwa kufanya ni kuwa kama simba mawindoni.

Unatakiwa ujue ni kundi gani la watu lipo tayari kushirikishwa fursa yako halafu ndio ung’ang’ane na ulikomalie kundi hilo tu mpaka kieleweke.

Ukifanya hivyo utaingiza watu sahihi kwenye fursa kiurahisi kabisa na...

Utaepuka vipingamizi (rejections) kutoka kwa watu ambao hawana uhitaji wa fursa yako.

Ungependa nikwambie makundi 2 ya watu ambao wapo tayari uwashirikishe fursa yako? Nilijuwa tu lazima utakubali.

Sasa kabla sijakwambia makundi hayo ni yepi naomba uniruhusu nikwambie kwanza makundi 5 ya watu ambao hata ufanye nini hawawezi wakajiunga kwenye fursa yako.

Watu hawa ukiwajua utaachana nao wasikupotezee muda na kukulaza njaa kama simba endapo angekuwa anamkimbiza mnyama mwenye mbio kali zaidi yake.

Makundi hayo 5 yapo kama ifuatavyo...

Kundi la kwanza: Waajiriwa waliolidhishwa na ajira zao!

Unajua kuna watu wanazipenda sana ajira zao kana kwamba wamelidhishwa na mshahara wanaoupata?

Pesa wanaoipata inawatosha kwa maisha wanayoishi kila siku.

Watu hawa mara nyingi hawana mpango wowote kwenye maisha yao wa kufanya kitu kingine tofauti na kuajiriwa.

Wengine kabisa hawajawahi kuwaza kumiliki biashara yoyote ile kwenye maisha yao.

Maisha ya kuamkia kwenye kiti cha ofisini na kutumikia ndoto za wengine kwake ndo maisha bora.

Kwahiyo ukiwashirikisha watu wa kundi hili utapata tabu sana.

Watakupa vipingamizi vya kila aina ilimladi tu uachane nao usiendelee kuwasumbua na fursa yako.

Rafiki yangu tunaelewana lakini?

Basi tuendelee na...

Kundi la pili: Watu wanaosema kuwa na pesa nyingi ni dhambi.

Hivi unajua kuna watu hawajawahi kuamini kama kwenye maisha haya unaweza ukatengeneza na kumiliki mamilioni ya pesa?

Niamini mimi watu hao wapo.

Watu hawa ukiwambia mamilioni ya pesa ambayo mtu anaweza akatengeneza kwenye fursa yako utaambulia kuambiwa kwamba huo ni “Ufreemanson”

Kaka yangu ni mfano wa kundi hili.

Nilipomshirikisha fursa hii aliniambia...

“Dogo achana na izo mambo ni ufreemanson mtupu”

Unaona? Watu hawa hata ufanye nini hawawezi wakajiunga kwenye fursa yako kwasababu wanaamini kuwa na pesa nyingi ni ushetani.

Tuendelee

Kundi la tatu: Kuna watu wana ujasiriamali ndani yao lakini hawaupendi mfumo wa biashara ya network marketing.

Hawa achana nao kabisa.

Kwasababu watakupasua kichwa.

Nisikilize kwa makini...

Kwenye dunia hii kuna aina na mifumo mbalimbali ya biashara.

Haimanishi biashara ya network marketing ndio biashara pekee ambayo watu wanatengeneza pesa.

Zipo biashara kibao ambazo watu wanatengeneza pesa kama wanazozitengeneza kwenye network marketing.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba...

Network marketing ni “kabiashara” kwenye kundi kubwa la biashara nyingi.

Ninachokimaanisha ni hiki...

Kuna mtu ukimwambia afanye network marketing atakwambia bora afe.

Lakini ukimwambia akauze viatu au nguo au mashuka atashangilia sana.

Kwanini?

Kwasababu haupendi mfumo wa biashara ya network marketing lakini anapenda mfumo wa biashara zingine.

Kiatu cha saizi moja hakiwezi kikatutosha sote.

Kwahiyo wapo ambao wanaupenda mfumo wa biashara hii lakini wapo wengine pia ambao hawaupendi.

Ni hawaupendi tu. Huwezi ukawalazimisha waupende kwa kumpaka nguruwe “lipstick”

Punguza kupiga makelele na mayowe kuhusu uzuri wa fursa yako.

Unapoteza muda wako bure kwa baadhi wa watu.

Umechoka? Mwenyewe nilijuwa tu hujachoka.

Tunaendelea

Kundi la nne: Watu ambao hawajawahi kuwaza kumiliki biashara yoyote kwenye maisha yao.

Ni kweli kuna watu kabisa wao hawajawahi kuwaza kumiliki biashara ya aina yoyote ile kwenye maisha yao.

Watu hawa wanaamini sana kwamba ajira ndio mpango mzima.

Pigia mstari. Usiwambie habari za biashara.

Ukithubutu tu. Utaishia kupata maumivu ya kukataliwa.

Asikudanganye mtu kwamba maumivu ya kukataliwa yanazoeleka.

Kukataliwa kila siku sio kunywa uji na vitumbua.

Wala sio kula nyama choma.

Kukataliwa kila siku ni sawa na kujilazimisha kutafuna mtishamba mchungu sana kila siku.

Hakuzoweleki.

Tuko pamoja mpaka hapo?

Vizuri. Ngoja tumalizie...

Kundi la tano: Watu ambao wana mafanikio na pesa za kutosha kwenye maisha yao.

Binadamu sio sawa na mbwa mwenye kuyarudia matapishi yake.

Ninachokimanisha ni hiki...

Mtu hawezi akawa ameshafanikiwa zake kimaisha. Kama ni pesa anazo halafu umwambie ajiunge kwenye fursa yako aanze msoto wa kuikuza biashara.

Ungelikuwa ni wewe ungeweza?

Usingeweza.

Lakini chakushangaza ni kwamba utakuta viongozi wakubwa wanakushauri utafute “Big fishes” (wenye hela zao) kwamba ukiwapata ni rahisi kuanza biashara.

Sio kweli.

Watu hawa kama ni pesa wanazo tayari.

Kama ni kutengeneza milioni 10 kwa wiki wanatengeneza na zaidi.

Sasa wewe unaenda kumwambia nini mtu wa namna hii.

Kwahiyo mtu ambae kafanikiwa kimaisha tayari sio sahihi kwa biashara hii ya network marketing.

Tambua kwamba...

Biashara ya network marketing ni daraja kwa ajili wa watu wenye uchumi wa hali ya chini kujikomboa kiuchumi.

Tunaelewana boss kubwa ajae?

Hayo ndo makundi 5 ya watu ambao hata ufanye nini hawawezi kujiunga kwenye fursa yako hata siku moja.

Sasa  kabla sijakwambia kundi la watu sahihi kushirikishwa fursa yako ngoja nikwambie sifa 3 ambazo kila mmoja wao anatakiwa kuwa nazo.

Sifa ya kwanza: Anatakiwa awe mtu mwenye ujasiriamali ndani yake.

Hii ni sifa ya kwanza anayotakiwa kuwa nayo mtu sahihi wa kumshirikisha fursa yako.

Kwasababu kama ana ujasiriamali ndani yake maana yake ashawahi kuwaza kumiliki biashara kwenye maisha yake.

Unakumbuka kuna kundi nimekwambia wao hawajawahi kuwaza kumiliki biashara yoyote kwenye maisha yao? Basi watu hao hawana ujasiriamali ndani yao.

Ndio maana nimekwambia hawafai kushirikishwa fursa yako vinginevyo utaishia kupata maumivu ya kukataliwa.

unanielewa lakini?

Basi tuendelee na...

Sifa ya pili: Anatakiwa awe mtu mwenye mapenzi na mfumo wa biashara ya network marketing.

Mtu anaweza akawa na ujasiriamali ndani yake lakini akawa hana mapenzi na mfumo wa biashara ya network marketing.

Kwahiyo kuwa na ujasiriamali ndani yake hakutoshi kumfanya awe mtu sahihi inatakiwa awe na mapenzi na biashara ya network marketing.

Mtu akiwa na mapenzi na mfumo wa biashara hii ni rahisi kujiunga kwenye timu yako.

Tukimalizia...

Sifa ya tatu: Anatakiwa awe ni mtu ambae ashawahi kufanya kipindi cha nyuma au anafanya kwa sasa biashara ya network marketing.

Mbona kama vile umeshituka?

Nisikilize kwa makini...

Networker mwenzako ni mtu sahihi wa kumshirikisha fursa yako endapo tu una ufunguo wa kumsaidia kufungua milango ya mafanikio yake.

Nadhani unaujua ugumu wa biashara hii.

Kwahiyo wapo networkers kibao ambao wameshaacha biashara na wengine wanaendelea kuhangaika wakisubiria siku ya kuacha biashara ifike.

Wewe ukiwaonesha watu hawa kuwa unayo njia ya pekee itakayowasaidia kupata mafanikio ambayo waliahidiwa siku ya kwanza walipoanza biashara basi watu hawa watakufata wenyewe na kuomba wajiunge kwenye timu yako.

Hivyo basi kwa sifa hizo 3 nilizokupatia tunapata makundi 2 ya watu ambao ni sahihi wewe kuwashirikisha fursa yako.

Kundi la #1: Networkers wenzako!

Huyu ni mtu sahihi kwasababu anaupenda mfumo wa biashara ya network marketing vinginevyo asingeweza kujiunga.

Mtu huyu pia yupo tayari kuoneshwa njia sahihi itakayomsaidia yeye kufikia malengo yake.

Kwahiyo kama simba akiwa mawindoni inatakiwa mtu huyu umkimbize na kumgeuza kitoweo.

Chondechonde mtu huyu usije ukajiroga ukaanza kusifia kampuni yako na kuiponda kampuni yake.

Hapo unakuwa unatengeneza uadui na sio urafiki.

Hapo juu nimekwambia kwamba kumpata networker mwenzako inatakiwa uoneshe ujuzi na uwezo wako katika kumsaidia yeye kutimiza malengo yake.

Ukiweza kufanya hivyo watakufata wenyewe na kuomba wajiunge kwenye timu yako.

Tumalizie

Kundi la #2: Watu ambao wanatalajia kuanza biashara ya network marketing.

Hivi unajua wapo watu wengi ambao wanatamani kufanya biashara ya network marketing lakini kulingana na hali ya biashara hii kuonekana kuwa ngumu wanasita kuanza biashara?

Watu hao wapo wengi tu.

Tena wengine wanahudhuria mikutano ya makampuni tofauti tofauti wakidhania wanaweza wakapata sehemu yenye uahueni wa kupata mafanikio.

Watu hawa ukiwaonesha njia sahihi itakayowasaidia wao kufikia malengo yao watajiunga kwako bila kuchelewesha.

Inatosha kwa leo.

Yours truly,

Mr Bokko!

P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.

P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.

Related Posts

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Mr Bokko


Mr Bokko ni Social Media Marketing & Advertising Expert + Founder & CEO wa Online Marketing System Pro Co Ltd - Kampuni yenye kuwasaidia Wafanyabiashara na Wajasiriamali njia rahisi ya kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni (Facebook & Instagram) kuweza kunasa wateja pasipo kupoteza muda na pesa kwenye njia ambazo hazifanyi kazi.

Your Signature

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}
>
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications