• Home
  • |
  • Blog
  • |
  • Je Na Wewe Unafanya Kosa Hili Kwenye Biashara Yako Ya Network Marketing?

August 21, 2022

Je Na Wewe Unafanya Kosa Hili Kwenye Biashara Yako Ya Network Marketing?

Post hii unatakiwa uisome mara mbilimbili.

Kwasababu niko naenda kukwambia kosa ambalo networkers karibia wote wanalifanya.

Kosa hili ndo chanzo kikubwa cha networkers wengi kushindwa kupata mafanikio kwenye biashara ya network marketing.

Ikiwa na wewe hutoliepuka kosa hili basi itakuwa ngumu sana kwako kupata mafanikio na kufikia malengo yako.

Lakini usijali ukiwa na mimi hapa rafiki yako Mr Bokko hutakiwi kuhofia kitu.

Leo naenda kukufundisha namna ya kuliepuka kosa hilo ili uanze kupata mafanikio na kufikia malengo yako haraka iwezekavyo.

Sasa kaa mkao wa kujifunza kwa maana darasa matata linaanza hivi punde.

Upo tayari?

Twende kazi.

Unahisi mtu anayeuza magodoro biashara yake ni ipi?

Umesemaje au nimesikia vibaya!

Kwamba yupo kwenye biashara ya kuuza magodoro?

Kosa kubwa sana hilo.

Mtu anayeuza magodoro biashara yake sio kuuza magodoro.

Biashara yake ni kuuza usingizi mzuri.

Nisikilize kwa makini rafiki yangu kipenzi...

Mtu anapoenda dukani kununua godoro anachokiwaza sana ni kupata godoro ambalo litadumu na litampatia usingizi mzuri usio na maumivu ya aina yoyote ile.

Mtu huyu hataki kujua vitu vilivyotumika kulitengeneza godoro. Anachotaka kuhakikishiwa ni uimara wa godoro na uhakika wa kupata usingizi muruwa kabisa.

Kwisha habari.

Kwahiyo kama mfanyabiashara wa magodoro biashara yako wewe sio kuwauzia watu magodoro bali ni kuwauzia watu uimara wa magodoro na usingizi mzuri.

Ukiweza kufanya hivyo utauza sana mpaka hutoami.

Turudi kwenye network marketing.

Networkers wengi wapo kama wauza magodoro kwasababu hawajui biashara wanayoifanya wao ni ipi.

Labda nikuulize...

Biashara yako wewe  kama networker ni ipi?

Siunaona? Nilijua tu hata wewe hujui biashara yako ni ipi.

Eti biashara yako ni kuuza bidhaa na kuingiza watu kwenye fursa.

Hili ndo kosa ambalo networkers wengi wanalifanya.

Hawajui wapo kwenye biashara gani.

Kuuza bidhaa na kuingiza watu kwenye fursa sio biashara yako.

Biashara yako ni nini sasa? Subiri kidogo nitakwambia hapo mbele muda si mrefu.

Tazama, wewe na wengine wote mliopo kwenye kampuni moja mna kitu kimoja cha kufanana.

Kitu hicho ni kwamba...

Nyote mmepewa fursa.

Sasa...

Inakuwa ngumu kujenga team kwasababu wewe na wengine wote mnakomaa kila iitwayo leo kuitangaza hiyo fursa moja ukidhania ndio biashara yako!

Maelfu ya watu mnatangaza kitu kimoja.

Kwasababu hiyo lazima iwe ngumu kupata watu wakujiunga maana nyote mnatangaza kitu kile kile ambacho watu wamezoea kukisikia kila siku.

Ndio maana unaalika watu hawaji kwasababu wanajua unachowaitia ni nini kabla hata hawajafika.

Tazama...kama nyote mnatangaza fursa moja, una kipi cha tofauti cha kumfanya mtu achague kujiunga kwako na sio kwa mtu mwingine au kampuni nyingine?

Au unadhani ubora wa kampuni uliyopo ndo utafanya watu wajiunge kwa sana? Kama ni hivyo mbona bado huna team kubwa? (Nisamehe kama nimekufokea lakini huo ndio ukweli)

Nisikilize kwa makini...

Unahangaika kujenga team kwasababu hujui biashara yako ni nini. Matokeo yake unajikuta unafanya vitu ambavyo kila mtu kwenye kampuni uliyopo anavifanya na mwisho wa siku unakuwa huna sababu ya kumfanya prospect atake kujiunga kwenye team yako.

Sasa tega masikio yako vizuri nikwambie biashara yako ni nini.

Biashara yako ni WEWE!

Ndio hujanisikia vibaya.

Nimesema hivi... biashara yako ni wewe mwenyewe.

Kivipi sasa? Iko hivi...

Kwenye biashara ya network marketing: watu wanajiunga kwa watu na sio kwenye kampuni.

Kwa maelezo mengine ni kwamba mtu anapokuja kuanza biashara anajiunga kwako wewe na sio kwenye kampuni.

Kwahiyo kama anajiunga kwako na sio kwenye kampuni anachokiangalia sana ni wewe na sio kampuni.

Kwa maana hiyo wewe ndio bidhaa inayonunuliwa na sio fursa ya kampuni yako.

Hivyo basi inabidi uelewe kwamba mpaka mtu anatoa pesa yake ajiunge kwenye team yako tambua kwamba hana agano au mkataba wowote na kampuni hiyo.

Kilichomfanya ajiunge kwako ni kwamba kuna vitu unavyo (Kichwani na sio mfukoni) ambavyo na yeye anatamani awe navyo au avijue ndio maana anajiunga ili umgawie japo kidogo au vyote kabisa.

Usikaze kichwa rafiki.

Ni rahisi kuelewa... Yani prospect wanakununua wewe na sio hiyo fursa.

Kwahiyo kuanzia leo unatakiwa ujue kwamba biashara yako wewe ni wewe mwenyewe na sio fursa yako.

Wewe ndio bidhaa ya biashara yako.

Sasa inabidi ujiulize...

Wewe ukiwa kama bidhaa ya biashara yako una lipi la kumfanya prospect atake kukununua?

Hapa sasa ndo unakuja usemi usemao “Sasa sijui inakuaje

Haya ngoja nikujibu.

Inakuwa hivi...

Kwakuwa wewe ndio bidhaa ya biashara yako....Na prospects wanakununua wewe basi unatakiwa uwe wa tofauti kabisa kwenye kampuni yako.

Na utofauti ninaouzungumzia ni kuwa na maarifa ya kipekee ya kuifanya biashara hii kitofauti kabisa.

Kwahiyo badala ya kutangaza fursa kama wengi wanavyofanya wewe unatakiwa utangaze uwezo wako wa kuweza kumsaidia mtu kutengeneza hela ndani ya muda mfupi pasipo kutumia nguvu nyingi.

Ukiweza kufanya hivyo nakwambia watu wengi sana wataanza kukukimbilia wajiunge kwenye team yako.

Unajua kwanini?

Kwasababu utaonekana ufunguo wa mafanikio yao hivyo watakusaka popote utakapokuwa hata kama ni uvunguni ili tu uwaingize kwenye team yako.

Prospects hawana utofauti na wana wa Israel huko Misri. Wapo kwenye mahangaiko na mateso makubwa.

Wanamtafuta Mussa (Kiongozi) ambaye atawaongoza kufika Nchi ya ahadi.

Kwahiyo ukijitokeza ukawa Mussa mwenye njia rahisi na ya haraka ya kuwasaidia wao kufikia malengo yao basi umasikini kwenye ukoo wako utakuwa umeisha maana watajiunga kwako kama utitiri.

Kwa leo ngoja niishie hapo.

Sincerely yours,

Mr Bokko.

P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.

P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.

Related Posts

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Mr Bokko


Mr Bokko ni Social Media Marketing & Advertising Expert + Founder & CEO wa Online Marketing System Pro Co Ltd - Kampuni yenye kuwasaidia Wafanyabiashara na Wajasiriamali njia rahisi ya kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni (Facebook & Instagram) kuweza kunasa wateja pasipo kupoteza muda na pesa kwenye njia ambazo hazifanyi kazi.

Your Signature

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}
>
Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications