• Home
  • |
  • Blog
  • |
  • Kipi Ukitangaze kati Ya Fursa au Bidhaa? Jibu Lake Litakushangaza!

August 21, 2022

Kipi Ukitangaze kati Ya Fursa au Bidhaa? Jibu Lake Litakushangaza!

Darasa hili utalipenda.

Kwasababu utajifunza kuepuka kosa ambalo linawafanya networkers wengi washindwe kupata downlines wapya kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Tazama...

Networkers wengi hawajui ni kipi wanatakiwa wakitangaze mtandaoni kati ya fursa na bidhaa.

Matokeo yake wanajikuta wanafanya kosa ambalo linawafanya washindwe kupata watu wapya wa kujiunga kwenye fursa.

Ukiniuliza ni kipi kati ya fursa au bidhaa unatakiwa ukitangaze mtandaoni...

Nitakujibu hutakiwi kutangaza chochote kati ya hivyo vitu 2.

Kwasababu unatakiwa uelewe kwamba hakuna mtu anayeingia mtandaoni kutafuta fursa ya kujiunga au bidhaa za kununua.

Au wewe kuna siku ushawahi kuingia mtandaoni ukiwa na wazo la kwenda kununua chochote kitu?

Jibu ni hapana.

Kwahiyo hata prospects zako unaowataka hawaingiagi mtandaoni kutafuta bidhaa za kununua au fursa ya kujiunga.

Kama hawaingii kununua au kutafuta fursa wanaingia kufanya nini?

Swali zuri sana.

Jibu lake ni rahisi.

Watu wakiingia mtandaoni wanaingia kufanya mambo 3 tu.

Mambo hayo 3 ni haya...

Jambo la kwanza: Kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki.

Mawasiliano ni moja ya hitaji kubwa kwetu sisi binadamu.

Isitoshe lengo kubwa la kuanzishwa kwa mitandao hii ya kijamii ni kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kuigeuza dunia kuwa kiganjani mwako.

Kwahiyo kitu cha kwanza ambacho mtu anakifanya aingiapo mtandaoni ni kuwasiliana na watu wake wa karibu.

umenipata vizuri hapo?

Safi. Basi tuendelee...

Jambo la pili: Kuchangia fikra, mawazo, mtazamo na hisia.

Mtu anapopost kitu fulan kwenye profile yake ya Facebook maana yake anachangia fikra zake, mtazamo wake, mawazo yake au hisia zake.

Kwahiyo hilo ni jambo la pili ambalo watu wanalifanya wakiwa mtandaoni.

Tukimalizia...

Jambo la tatu: Kutafuta dondoo mpya ya vitu ambavyo wanamapendeleo navyo.

Kila mtu ana mapendeleo yake.

Kuna mtu mapendeleo yake ni mpira. Kwahiyo akiingia mtandaoni atatafuta dondoo mpya kuhusu mpira.

Kuna mtu mapendeleo yake ni siasa. Kwahiyo akiingia mtandaoni atatafuta dondoo mpya za siasa kutoka kwa Kigogo na wana siasa wengine wakubwa.

Kuna wengine mapendeleo yao ni muziki. Kwahiyo wakiingia mtandaoni wanatafuta dondoo mpya kuhusu muziki.

Kwahiyo kutafuta taarifa mpya juu ya kitu ambacho mtu ana mapendeleo nacho ni jambo la tatu ambalo mtu anaingia kulifanya mtandaoni.

Kama unavyoweza kuona hakuna sehemu nimesema kwamba watu wanaingia kununua au kutafuta fursa ya kujiunga.

Sasa kama watu hawaingii mtandaoni kununua bidhaa au kujiunga kwenye fursa utafanyeje ili upate prospects wa kujiunga kwenye timu yako?

Swali zuri sana.

Jibu lake mbona rahisi tu.

Kabla sijakwambia jibu lake tupate mapumziko kidogo.

Chukua glass ya maji kunywa maji yako taratibuuu huku ukisikiliza stori hii ninayoenda kukusimulia.

Stori hii ni ya ukweli kabisa.

Inanihusu mimi.

Hivi kwenye maisha yako imeshawahi kutokeo ukakutana na mtu ndani ya muda mfupi ukajikuta umempenda?

Penzi zito.

Basi bwana miaka kadhaa iliyopita nilikutanaga na mdada mmoja mzuri nikajikuta nimezama kwenye penzi zito ndani ya muda mfupi.

Ilikuwa rahisi kupata mawasiliano ya mdada huyu kwasababu alikuwa ni rafiki wa mdada fulani ninaefahamiana nae.

Kumpenda mtu ni kuzuri jaman.

Lakini kuna mawili. Kupendwa na wewe au kutopendwa.

Nikaamua kuvunja ukimya nimwambie ukweli mdada huyu kwamba nimemuelewa.

Jibu nililopewa ndugu yangu hata makamasi ni masafi.

Ona unavotamani kulijua jibu hilo.

Sikwambii ng’oo.

Baada ya kupewa jibu hilo mdada huyu hakuishia hapo.

Akapost kwenye status yake whatsapp kwamba...

“You can’t be handsome and broke at the same time, you better choose one”

Ijapokuwa hakuonesha anamlenga nani lakini nilijua kanilenga mimi kwasababu alipost siku moja baada ya mimi kumwaga sera zangu kwake.

Jamani jamani kwamba...

Huwezi ukawa handsomeboy halafu ni kapuku ni afadhali uchague kuwa kapuku uhandsome uweke pembeni au uwe na pesa ndo uwe handsome.

Hehehehe kwa mtazamo wako unahisi niliumia au sikuumia?

Jibu baki nalo mwenyewe.

Tuendelee na darasa letu. Muda wa pumziko umeisha.

Kwanini nimekusimulia stori hii?

Sijataka uburudike tu.

Kuna funzo pia nimelenga ulipate.

Funzo hilo ni kwamba kama inawezekana kuingia kwenye penzi zito kwa mtu ambae umemjua ndani ya muda mfupi basi...

Ni rahisi pia kuwafanya prospects zako waanguke kwenye penzi zito na fursa yako na mwisho wa siku wakupatie pesa kwa haraka ili wajiunge kwenye timu yako.

Inawezekana sana.

Endapo tu utafanya hivi...

Kwa mfano unakimbizwa na Simba mwenye njaa Kali.

Unatimuka mbio za ajabu ambazo hujawahi Kwenye maisha Yako Maana ukizembea tu Simba anakugeuza kitoweo!

Kwa bahati mbaya unavyozidi kukimbia, mbele unakutana na Mto mpana Sana usio na daraja na Ndani ya Mto huo Kuna mamba wakali Sana wenye njaa.

Kwahiyo huna chaguo. Ukisimama Simba lazima akugeuze kitoweo. Ukiruka lazima udumbukie mtoni na kumbuka Kuna mamba wakali wenye njaa kwahiyo lazima tumbo la mamba ligeuke kuwa kaburi lako.

Maswali 2 yanakuja...

1. Hapo hitaji lako ni Nini? Na

2. Kikwazo kinachosababisha wewe usipate hitaji lako ni kipi?

Jibu la swali la kwanza: Hitaji lako ni kuvuka kwenda upande wa pili ili Simba asikugeuze kitoweo

Hitaji lako Sio daraja.

Daraja ni nyenzo tu ya kukusaidia wewe upate Hitaji lako la kwenda upande Wa pili Wa Mto.

Ikitokea mtu akisema ukijing’ata ulimi utajikuta upande wa pili lazima ufanye hivyo.

Kwahiyo daraja sio hitaji lako. Unachokihitaji wewe ni usalama wa maisha yako. Usalama huo unapatikana upande wa pili na sio kwenye daraja.

Jibu la swali la pili: Kikwazo kinachosababisha wewe usipate hitaji lako ni ukosekanaji wa daraja.

Kwahiyo ili uweze kufika upande wa pili inatakiwa uondokane na Kikwazo Cha ukosekanaji wa daraja.

Mfano Huu unamaanisha Nini?

Mfano Huu unachokimaanisha ni hiki...

Hakuna prospects mwenye uhitaji wa fursa yako. Hata wewe ulivyojiunga hitaji lako halikuwa fursa.

Ulivyojiunga ulikuwa na malengo yako uliyotamani uyatimize kupitia fursa hiyo.

Malengo hayo uliyotamani kuyatimiza ndio HITAJI lako wewe na sio fursa.

Fursa ni baadhi ya nyenzo za kukusaidia kutengeneza daraja tu la kukuwezesha wewe kuyafikia malengo yako.

Naomba nieleweke vizuri, fursa yako sio hitaji lako na wala sio daraja.

Bali ni baadhi ya nyenzo za kukusaidia kutengeneza daraja la kukuwezesha wewe kuyafikia malengo yako.

Nikisema fursa ni baadhi ya nyenzo maana yake nyenzo hazijakamilika kuweza kutengeneza darasa zima. Zinahitajika nyenzo zingine ndio daraja likamilike.

Nyenzo hizi zilizokosekana zisipopatikana daraja la kukuwezesha kufikia malengo yako litakosekana na hivyo utaliwa na simba au mamba ndani ya mto (Utashindwa kupata hitaji lako)

Usikaze kichwa. Legeza kichwa halafu fikiria mfano wa kukimbizwa na simba niliokutolea hapo juu utaelewa vizuri ninachokimaanisha.

Unadhani kwanini bado hujafikia malengo yako licha ya kuwa ushajiunga kwenye fursa tayari?

Kwasababu kuna ukosekanaji wa daraja ambacho ni kikwazo kinachokuzuia wewe kushindwa kutimiza malengo yako.

Ukosekanaji wa daraja unasababishwa na kukosekana kwa nyenzo zilizobaki kukamilisha utengenezwaji wa daraja.

Nyenzo hizo zilizokosekana ni nini?

Nyenzo hizo ni...

Mbinu sahihi za kupata watu wakujiunga kwenye fursa.

Nisikilize kwa makini...

Wewe hapo unahangaika mpaka leo hii kutimiza malengo yako kwasababu hujui mbinu sahihi za kupata prospects wa kujiunga kwenye fursa.

Mbinu hizo ungekuwa unazijua leo hii ungekuwa ushatimiza malengo yako mengi na usingekuwa unaendelea kutanga tanga na kuhangaika kupata watu wakujiunga kwenye fursa yako.

Kwahiyo kukosekana kwa mbinu hizi kunafanya kuwepo na ukosekanaji wa daraja la kukuvusha ufikie malengo yako.

Kwahiyo sasa...

Hata prospects wana malengo yao ambayo wanatamani kuyatimiza kwenye maisha yao.

Inatakiwa utambue kwamba prospects unaowataka wajiunge kwenye fursa yako watakutegemea wewe ndio uwaoneshe daraja la kuwasaidia wao kutimiza malengo yao.

Sasa utawaoneshaje wakati wewe mwenyewe hicho ndicho kikwazo kinachokuzuia wewe ushindwe kutimiza malengo yako?

Hapo ndipo ugumu wa kupata watu wa kujiunga kwenye fursa yako unapoanzia.

Unajua siri ya kupata watu wengi wakujiunga kwenye fursa yako imejificha wapi?

Imejificha kwenye mbinu sahihi za kupata watu wa kujiunga kwenye fursa yako.

Networkers wengi wanaacha biashara kwasababu ya kukosekana kwa mbinu sahihi za kupata watu wa kujiunga kwenye fursa.

Kama ni hivyo huoni wewe ikitokea ukazijua mbinu hizo sahihi tayari unakuwa na ufunguo wa mafanikio ya networker wenzako wote na mtu yeyote anayetaka kujiunga kwenye fursa?

Ukizijua mbinu hizo sahihi tayari daraja linakamilika kupitia wewe kwahiyo mtu ana uhakika akijiunga kwako lazima atimize malengo yake.

Kumbuka nimekwambia hitaji lako au la networker mwenzako sio fursa.

Kwahiyo ukiwa na mbinu hizo sahihi unageuka kuwa sumaku. Prospects wanakutafuta wenyewe uwaunge kwenye fursa yako.

Sasa...

Tukirudi kwenye swali letu...

Sasa kama watu hawaingii mtandaoni kununua bidhaa au kujiunga kwenye fursa utafanyeje ili upate prospects wa kujiunga kwenye timu yako?

Mpaka sasa hivi nina imani ulishalijua jibu la swali hili.

Kama bado basi jibu lake ni hili...

Unachotakiwa kwenda kutangaza mtandaoni ni utatuzi wa kikwazo kinachofanya prospect wako ashindwe kutimiza malengo yake endapo atajiunga kwenye timu yako.

Utatuzi huo ni elimu ya BURE ya kumsaidia prospect aweze kukiepuka kikwazo ambacho kitazuia yeye kutimiza malengo yake.

Kwa maelezo rahisi ni kwamba...

Tangaza kutoa elimu ya bure ya kutumia mitandao ya kijamii kupata watu wa kujiunga kwenye fursa (Mbinu sahihi)

Unadhani mtu anayetaka kujiunga kwenye biashara ya network marketing akiliona tangazo hilo ataacha kutaka kupata elimu hiyo ya BURE?

Lazima aitake elimu hiyo ya bure.

Lakini wewe sio mjinga.

Elimu hiyo ya bure unayoitoa sio kila kitu unachokijua.

Unatoa kionjo tu cha kumtamanisha prospect kutaka kujua zaidi.

Kwa kufanya hivyo prospect atakuamini, atakupenda haraka na atatamani umshike mkono atimize malengo yake.

Ukitoa kionjo hicho halafu ukamwambia ili kupata elimu nzima inatakiwa ajiunge kwenye timu yako unadhani kitakachotokea ni kipi? Jibu unalo tayari.

Ndio sio wote watakaojiunga kwa haraka lakini unadhani ambae hatajiunga ataendelea kuhangaika mpaka lini wakati ufunguo wa mafanikio yake unao wewe?

Lazima na yeye mwisho wa siku ajiunge tu kwenye timu yako.

Sicerely yours,

Mr Bokko! 

P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.

P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.

Related Posts

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Kipi Bora, Kuuza au Kuingiza Watu Kwenye Fursa?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Ni Kosa La nani Downline wako akiquit?

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Sababu 1 Pekee Ya Kumfanya Ajiunge Kwako Na Sio Kwa Mtu Mwingine!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Ukifanya hivi prospects wataipenda Fursa Yako!

Mr Bokko


Mr Bokko ni Social Media Marketing & Advertising Expert + Founder & CEO wa Online Marketing System Pro Co Ltd - Kampuni yenye kuwasaidia Wafanyabiashara na Wajasiriamali njia rahisi ya kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni (Facebook & Instagram) kuweza kunasa wateja pasipo kupoteza muda na pesa kwenye njia ambazo hazifanyi kazi.

Your Signature

  • {"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}
    >
    error: Content is protected !!
    Powered by ProofFactor - Social Proof Notifications