Nimekuwa nikiulizwa swali hili mara kwa mara kwamba...
Downline wako anapoacha biashara (Akiquit) nani alaumiwe –downline au upline?
Au wakati mwingine naulizwa downline anapoquit ni kosa la nani?
Swali hili ni gumu sana kwa mtu ambae hajui anachokifanya kwenye biashara yake na hajui kuhusu “The law of attraction”
The law of attraction inasema...
“You attract what you are”
Kwa lugha rahisi ni kwamba...
“Ndege wafananao huruka pamoja”
Ninachokimaanisha ni kwamba...
Downline kuacha biashara ni kosa la wote.
Ni Kosa la downline mwenyewe na ni kosa na upline pia.
Ngoja tuanze na upline.
Downline anapoacha biashara ni kosa lako kwasababu pindi anaanza biashara alichagua kujiunga kwako akidhania kupitia wewe itakuwa rahisi kwake kutimiza malengo yake.
Na isitoshe ulimuahidi kumpatia sapoti ya kutosha mpaka yeye kufikia malengo yake.
Lakini baada ya kuanza biashara mambo yapo tofauti kabisa.
Sapoti aliyotegemea kupewa haipati.
Mafunzo aliyotegemea kuyapata kutoka kwako hayaoni.
Kila unachomuelekeza kufanya hakimpatii matokeo yoyote yale.
Kwahiyo ulitumia uongo na ujanja ujanja kumfanya ajiunge kwako lakini kiukweli huna mbinu za kumsaidia yeye kufikia malengo yake.
Kwa lugha rahisi wewe ni tapeli.
Haiwezekani umwambie akijiunga utampatia mafunzo na sapoti ya kutosha halafu baada ya kujiunga unampotezea kwahiyo akiacha biashara linakuwa ni kosa lako.
Na sababu nyingine ambayo inafanya kuacha biashara downline wako kuwe kosa lako ni...
Wewe kuwa na tamaa ya kutaka kila mtu ajiunge kwenye team yako.
Matokeo yake unajikuta unaingiza kwenye team yako mijitu mivivu, milalamikaji ambayo inaishia kutofanya kazi yoyote.
Lakini kama nilivyosema sio kosa lako mwenyewe. Ni kola la wote. Tumemaliza kuona sababu ya kwanini ni kosa lako.
Sasa tuone sababu ya kwanini ni kosa la downline mwenyewe.
Ni ukweli ulio wazi kwamba...
Biashara inachukuwa muda kujengwa.
Lakini chakushangaza watu wengi wanataka utajiri wa haraka.
Matokeo yake ni kwamba mtu wa namna hii anapoanza biashara mategemeo yake ni kuwa tajiri ndani ya kipindi kifupi.
Ikitokea mambo yakawa tofauti alivyodhania anakimbilia kuacha biashara.
Badala ya kuwa kama mimi anakimbilia kuacha biashara.
Tazama...
Ndani ya miaka 3 kwenye biashara hii niliweza kuingiza watu 2 tu kenye fursa.
Kwa mtu mwenye roho nyepesi angeshaacha biashara zamani sana.
Kwangu haikuwa hivyo.
Badala ya kukimbilia kuacha biashara nilipambana mpaka nikapata njia ambayo kwa sasa inaniwezesha mimi na team yangu kupata watu wapya 4-8 wakujiunga kwenye team kila wiki.
Swali...
Suluhisho la watu wengi kutoacha biashara kwenye team yako ni lipi?
Ahsante kwa swali lako zuri.
Suluhisho lake ni hili...
Kwanza: Pata maarifa sahihi ya kuifanya biashara ya network marketing.
Kwasababu bila maarifa sahihi utaishia kupata watu wavivu na wabovu kwenye team yako.
Unakumbuka the law of attraction inasemaje?
“You attract what you are.”
Kwahiyo usitegemee kupata mashine za kazi kwenye team yako wakati wewe mwenyewe sio mashine ya kazi.
Anza kwanza wewe kuwa mashine ya kazi halafu utaona jinsi ambavyo mashine za kazi zingine zitakavyojileta kwako.
Pili: Usimuingize kila mtu kwenye team yako.
Chagua kundi la watu unaowataka kwenye team yako.
Fanya hivyo utakuja kunipa mrejesho badae.
The end.
Yours truly,
Mr Bokko.
P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.
P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.