Usipoteze muda wako kusoma ujumbe huu kama sponsored ads zako bado zinakuletea matokeo mazuri. Lakini kama wewe ni mfanyabiashara ambaye sponsored Ads (FB & IG) zako hazileti matokeo mazuri kama zamani…
Ongeza Mauzo Zaidi Kwa Kutumia “Proof Ads” —Aina Mpya Ya Sponsored Ads Zinazoongeza Uhitaji Wa Bidhaa Yako Sokoni, Zinafanya Wateja Wakuone Bora Kuliko Wafanyabiashara Wenzako, na Hata Kuwageuza wateja Waliopo kuwa Washawishi Wa Kukuletea Wateja Wapya!

From: Mr Bokko
Ndugu mfanyabiashara,
Matangazo yako ya kulipia (Sponsored Ads) yanafanya vizuri? Kama jibu ni hapana, basi baada ya kusoma ujumbe huu unatakiwa uwe na uhakika 100% matangazo yako yanaanza kufanya vizuri na kukupatia matokeo makubwa zaidi.
Na hizi hapa sababu kuu 3 ambazo zinapelekea sponsored ads zako zisifanye vizuri kama ilivyokuwa hapo awali.
Kabla sijakwambia sababu hizo ni zipi, niruhusu niseme makundi ya wafanyabiashara ambao watanufaika na aina hii mpya ya sponsored ads ninayoenda kukufundisha na makundi ya wafanyabiashara ambao hawatanufaika.Makundi Ya Wafanyabiashara Ambao Hawatanufaika na Aina Hii Mpya Ya Sponsored Ads.
Wauza virutubisho lishe (Dawa): Watu hawa hawatanufaika kwa sababu badala ya aina hii mpya ya sponsored ads kuwasaidia kuongeza mauzo itakuwa kinyume chake: Mauzo yatapungua zaidi kwa sababu inawaaibisha wateja (Asilimia kubwa ya watu hatupendi kila mtu ajue matatizo yetu ya kiafya)
Wafanyabiashara ambao hawajawahi kufanya sponsored ads kabisa. Kama hujawahi kufanya sponsored ads kabla haijalishi unafanya biashara gani, aina hii mpya ya sponsored ads sio kwa ajili yako.
Kundi La Wafanyabiashara Ambao Watanufaika na Aina Hii Mpya Ya Sponsored Ads.
- Wafanyabiashara ambao sponsored ads zao zilikuwa zinafanya vizuri mwanzo lakini kwa sasa hazifanyi vizuri tena.
Sababu 3 Zinazofanya Sponsored Ads Zisifanye vizuri kama Ilivyokuwa Kipindi Cha Nyuma!
1.Ongezeko La Ushindani: Hapo mwanzo, ni wafanyabiashara wachache waliokuwa wanafanya sponsored ads, hivyo ushindani ulikuwa ni mdogo. Wateja hawakuona matangazo mengi yenye kuuza bidhaa za kufanana. Sasa, Ongezeko la wafanyabiashara wanaofanya sponsored ads limefanya mauzo kupungua kwa sababu saivi wateja wana machaguo mengi na wewe unaendelea kurusha matangazo kama mwanzo wakati soko limeshachafuka.
2.Gharama za matangazo kupanda juu: Kwa sababu ya kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaofanya sponsored ads, Meta (Fb & IG) wamepandisha gharama za matangazo maana platform yao inawaweka wafanyabiashara kwenye (Auction) —kinyanganyiro ambapo mwenye bajeti kubwa zaidi ndo anapata matokeo mazuri. Na mwenye bajeti kidogo anapata matokeo kidogo au hapati kabisa. Ndio maana hapo mwanzo ulikuwa unaweza kutumia bajeti ya dola 3-5/siku ukapata matokeo mazuri lakini kwa sasa mambo yamebadilika sana.
3.Wateja wamekuwa “Comparison shoppers”: Kwa sababu kuna sponsored ads nyingi zinazotangaza bidhaa za kufanana kutoka kwa wafanyabiashara tofauti, wateja hawanunui haraka kama ilivyokuwa hapo awali badala yake wanaanza kulinganisha bidhaa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja na mwingine. Mfanyabiashara mwenye jina na ambaye inaonekana ni bora ndiye atakaye shinda na kupata wateja wengi.
Kama umekuwa ukirusha sponsored ads kama zamani tambua kwamba sasa ni wakati wa kubadilisha aina ya sponsored ads zako vinginevyo utaendelea kupoteza pesa nyingi bila matokeo mazuri kwa sababu hizo 3 nilizoelezea hapo juu.
Taarifa njema? Kuna aina mpya ya sponsored ads inayoitwa “Proof Ads” ambayo:
Jinsi Nilivyotengeneza Dola 32,900 (85,540,000) Ndani Ya Siku 30 Kwa Kutumia “Proof Ads”
Mwaka 2023 mwishoni nilianza kuuza digital products Marekani, Canada, Australia na nchi za Ulaya.
Ilikuwa ni safari yenye changamoto kubwa, maana nilitegemea kupata wateja kupitia matangazo ya kulipia (Sponsored Ads) Facebook na Instagram.
Lakini tatizo ni kwamba kwenye nchi hizo ushindani ni mkubwa mno — mamilioni ya wafanyabiashara wanatumia matangazo ya kulipia, hivyo kufanya gharama za kutangaza kwenye nchi hizo kuwa juu kupita kiasi.
Kwa mfano: Ukiweka bajeti ya dola 50 kwa siku, tangazo lako linaweza kuonekana kwa watu 500–1500 tu. Lakini hapa Tanzania, bajeti hiyo hiyo tangazo lako linaonekana kwa zaidi ya watu 30,000!

Sasa, faida ya masoko ya nje ni kwamba “buyer intent” yao ni kubwa sana. Hata kama wanaona tangazo wachache, thamani yao ni kubwa kiasi kwamba unaweza kufanya mauzo makubwa.
Hata hivyo, ukweli mchungu ni huu:
Ushindani ukiwa ni mkubwa sanaa meta (Facebook & Instagram) anapandisha gharama za kulitembeza tangazo lako kwa watu wengi.
Kwa hiyo ikawa inanilazimu nitumie bajeti kubwa ili meta alitembeze tangazo langu lionekane kwa watu wengi.
Matokeo yake? Kipato changu kilikuwa cha kupanda na kushuka kila wakati.
Kuna wakati nilikuwa napata hasara kubwa sana.
Kuna wakati nilikuwa napata hasara kidogo na
Kuna wakati nilikuwa napata faida nzuri.
Nilipambana sana, lakini hali hii ya kipato kupanda na kushuka mara kwa mara iliendelea hadi kufikia Januari 2025.
Kwenye kipindi hiki cha kuanzia mwishoni mwa 2023 hadi Januari 2025, nilijikuta nikinunua kozi nyingi sana. Kwa sababu niliamini lazima kuna njia bora zaidi ya kufanya sponsored ads zifanye vizuri zaidi kwenye soko lenye ushindani mkubwa.
Kila kozi ilinipa matumaini mapya ya kupata suluhisho la kudumu. Lakini kila mara matokeo yalikuwa yale yale…
Bajeti kubwa, faida ndogo.
Au wakati mwingine kabisa, hasara tupu.
Nilikuwa nimechoka. Nilihisi kama nipo kwenye mbio za panya zisizoisha. Kila siku nikijiuliza: “huenda biashara hii hainifai nalazimisha maji kupanda mlima?”
Hata zile kozi nilizonunua kwa maelfu ya dola hazikutoa majibu niliyokuwa natafuta. Ilifika hatua nikaanza kufikiria kuachana kabisa na soko hili.
Lakini ndipo ikafika Januari 2025 — mwezi ulioandika historia mpya kwenye safari yangu. Mwezi ambao uligusa “reset button” ya kila kitu nilichokuwa napambana nacho.
Tazama, nilikuwa nimefika hatua ya mwisho ya uvumilivu wangu. Nikiwa nimechoka kiakili na kifedha, nilianza kufikiria kuacha kabisa mambo ya sponsored ads kwenye soko hili la nje.
Lakini kuna kitu kimoja kilinikosesha kabisa amani.
Kulikuwa na aina fulani ya matangazo niliyoyajua, na hata nilifahamu jinsi ya kuyarusha. Sio hivyo tu — niliwahi kuona baadhi ya watu wakiyatumia.
Lakini kila mara mimi binafsi nilikuwa nayabeza. Nilijiambia: “Matangazo ya namna hii hayawezi kufanya kazi kwenye soko lenye ushindani mkubwa namna hii. Huu ni upuuzi mtupu.”
Kwa sababu hiyo sikuwahi hata kuyajaribu. Nilihisi kama ni kupoteza muda.
Lakini kwa hatua niliyokuwa nimefika, nilijiambia: “Nina nini cha kupoteza sasa? Nimejaribu kila kitu kingine. Labda ni wakati wa kujaribu kile nilichokuwa nakiweka kando siku zote.”
Wakati najiandaa kujaribu aina hiyo ya matangazo, nilikumbuka somo moja muhimu sana nililojifunza kwenye kozi ya mwisho niliyonunua. Kozi ile ilifafanua kwa undani jinsi kampuni kubwa duniani kama Apple na Amazon zinavyouza bidhaa zao si kwa kutegemea bajeti kubwa pekee, bali kwa kutumia mbinu ya kisaikolojia yenye nguvu ya ajabu: Social Proof na FOMO.
Nikaanza kuelewa kwa nini yale matangazo niliyokuwa nayabeza kumbe ndiyo yana siri kubwa ya kufanya kazi hata kwenye soko lenye ushindani mkubwa.
Ngoja nikuelezee jinsi mbinu hiyo ya kisaikolojia inavyotumika:
Tuanze na kampuni ya Apple.
Kila mara Apple inapokaribia kuzindua iPhone mpya, kuna jambo la ajabu linalojirudia. Siku chache tu kabla ya tarehe rasmi ya kuanza kuuza, kampuni hufungua mlango kwa wateja wachache waliopo karibu na maduka yao makuu.
Lakini lengo lao si tu kuuza simu. Hapana. Lengo lao ni kutengeneza taswira.Taswira ya maelfu ya watu wakipanga mistari mirefu, wakiwa na macho yenye shauku, wakingoja kushika toleo jipya.
Kamera zinafanya kazi yake. Picha na video za foleni zisizoisha husambaa duniani kote. Kila mtu anaona. Kila mtu anashuhudia.
Ndipo hapo “Social Proof” huchukua nafasi yake — ushahidi wa kijamii unaosema: Kama watu wengi wanakitaka, basi ni lazima kitu hiki kina thamani kubwa.
Na hapo ndipo FOMO — Fear of Missing Out, hofu ya kupitwa — huanza kutikisa nafsi za mamilioni ya watu. Hata yule ambaye hakuwahi kufikiria kununua iPhone mpya, ghafla anajikuta akisema: “Labda nami nahitaji hii simu… nisije nikapitwa.”
Kwa hivyo, si simu yenyewe pekee inayouza. Ni maelfu ya watu kwenye mistari. Ni picha. Ni simulizi. Ni nguvu ya kisaikolojia inayoitwa Social Proof — injini halisi ya kuonesha bidhaa ina “demand” kubwa.
Amazon nayo inatumia dhana hii ya social proof na FOMO kama ifuatavyo:
Ukiingia Amazon, si kila bidhaa ina nafasi sawa. Zingine huonekana na alama ndogo lakini zenye nguvu kubwa: “Best Seller” au “Trending Now.”
Alama hizi hazionekani kama mapambo tu. Ni silaha za kisaikolojia. Zinakufanya uamini: “Kama bidhaa hii ndiyo inayonunuliwa zaidi, basi ni lazima iwe bora zaidi.”
Kwa sekunde chache, akili yako hupata uthibitisho wa kijamii bila hata kuangalia maelezo zaidi. Watu wengi wameichagua tayari, na wewe hutaki kupitwa.
Hii ndiyo siri ya Amazon: haikupi tu bidhaa, inakupa ushahidi wa kijamii uliofungwa ndani ya nembo ndogo ndogo. Badges ndogo zinazoonekana kama taarifa zisizo na madhara, kumbe ndizo zinazobadilisha maamuzi ya mamilioni ya wanunuzi kila siku.
Na matokeo yake? Bidhaa iliyopewa alama ya “Best Seller” huendelea kuuza zaidi na zaidi — si kwa sababu tu ni bora, bali kwa sababu dunia nzima inaiona kama bora.
Naweza kuendelea kukupa mifano ya makampuni mengine kibao yanayotumia dhana ya “Social Proof na FOMO” kuuza mamilioni ya bidhaa zao, lakini kwa leo tuishie kwenye mifano hii miwili: Apple na Amazon.
Sasa turudi kwenye stori yangu —Baada ya kuelewa saikolojia hii kiundani zaidi nikaona kumbe matangazo ambayo nimekuwa nikiyabeza yanaweza kweli kufanya kazi. Na yinsi ya kutumia dhana ya “Social Proof na FOMO” kwenye matangazo haya ni kama ifuatavyo:
Unarusha aina fulani ya Sponsored Ads ambapo wito wako (Call to Action) ni kuwaambia watu wenye uhitaji wa kile unachouza wakomenti neno maalum ulilowaambia.
Kadri wateja wengi wanavyokomenti neno hilo maalum kwenye tangazo lako, ndivyo taswira ya “foleni ya uhitaji” inavyojengeka machoni pa wengine.
Kila komenti kwenye tangazo lako ni sawa na mtu mmoja aliyesimama kwenye mstari akisubiri bidhaa. Kadri komenti zinavyoongezeka, ndivyo inavyoonekana kuna uhitaji mkubwa wa kile unachokitangaza.
Na kama vile foleni za iPhone mpya au alama ya “Best Seller” ya Amazon, kila komenti kwenye tangazo lako ni ushahidi wa kijamii unaoonyesha kwamba bidhaa yako inahitajika sana.
Matokeo yake? Mauzo huongezeka kwa sababu watu huona thamani kupitia “foleni” ya komenti zilizojaa kwenye tangazo lako.
Ni kweli, si kila mtu atakayekomenti ataishia kununua bidhaa yako. Lakini kumbuka, lengo kuu ni kutengeneza picha kubwa (taswira) kwamba unachouza kina uhitaji mkubwa. Hapo ndipo wale waliokuwa bado wanajifikiria mara mbili wanajikuta wakiharakisha ili wasipitwe na fursa kabambe.
Kwa hiyo hata kama mtu akikomenti lakini akawa hajanunua, komenti yake bado ina thamani kubwa sana. Kwa sababu zinapokuwa komenti nyingi zenye neno maalum, kila komenti kwenye tangazo lako inageuka kuwa “alama ya ushahidi” inayowavuta na kuwaonesha wateja sahihi kwamba:Baada ya kuona jinsi nguvu ya Social Proof na FOMO inavyoweza kufanya kazi hata kwenye soko lenye ushindani mkubwa, niliamua kujaribu mbinu hiyo mara moja.
Hivyo, Mwezi wa pili mwaka 2025 nilianza kurusha aina ya matangazo ambayo yalitumia wito maalum (Call to Action) — ambapo ili mtu apate kile ninachokitangaza kwenye tangazo, inatakiwa akomenti neno maalum ambalo nitamwambia.
Kwa sababu ya dhana ya “Social Proof na FOMO” watu wengi sana wenye uhitaji walianza kukomenti kwa wingi.
Cha muhimu zaidi, nilikuwa nimeshaseti mfumo wa kiotomatiki uliokuwa unageuza komenti hizo kuwa mauzo masaa 24/7 — bila mimi kuhitaji kuchat na kila mmoja wao.
Matokeo yalikuwa ya kushangaza:

Ndani ya siku 30, yaani mwezi wa pili mwaka 2025, nilitumia dola 6700 (17,420,000) kama bajeti ya matangazo Facebook na Instagram kurusha aina hii ya matangazo.
Matokeo? Nikatengeneza mauzo ya jumla dola 32,900 (85,540,000). Faida yangu baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji ilikuwa dola 24,500 (63,700,000)
Matokeo haya ni kwa sababu ya kurusha aina hii ya matangazo yenye kutumia dhana ya “Social Proof na FOMO”
Na kuna kitu kingine nilichogundua:
Unapotumia aina hii ya matangazo, Meta hukupunguzia gharama za kulitembeza tangazo lako kwa watu wengi — kwa sababu algorithm yake inapenda engagement kubwa (likes, shares, comments).
Kwa maneno mengine, Social Proof si tu inaleta wateja, bali pia inafanya tangazo lako liwafikie watu wengi zaidi kwa gharama nafuu.
Pengine unauliza, “Je, nilikuwa nikiwageuza vipi waliokomenti kuwa mauzo?”
Naam, kama umefika hapa baada ya kukomenti kwenye tangazo langu, basi tayari umeshashuhudia mbinu hii ikifanya kazi kwa macho yako mwenyewe. Komenti yako ndiyo imekuleta hapa, na sasa una nafasi ya kulipia bidhaa yangu.
Na vivyo hivyo, ndivyo wateja wako watakavyofikishwa moja kwa moja kwenye OFA zako —kulingana na biashara yako ilivyo.
Nimekuwa nikitumia aina hii ya matangazo kwa siri licha ya wafanyabiashara wengi ninaofahamiana nao kuniuliza mara kwa mara jinsi gani naweza kuwasaidia sponsored ads zao kufanya vizuri kama hapo awali.
Lakini hatimaye nimeamua kuvujisha siri hii katika kozi yangu mpya ambayo nimeipa jina la “Proof Ads Hack”

Katika kozi hii fupi (ambayo unaweza kuimaliza ndani ya masaa 2 tu) utajifunza mambo 4 yafuatayo:
1. Jinsi ya kutumia ads manager kuseti “Proof Ads” — aina mpya ya matangazo inayotumia nguvu ya Social Proof na FOMO kukuondoa kwenye ushindani sokoni na kuongeza uhitaji wa bidhaa yako machoni pa wateja.
2. Maneno Maalum Ya Kukomenti —Haya ni maneno ambayo wateja wakikomenti kwenye tangazo lako, yanaongeza nguvu ya dhana ya “social Proof na FOMO” hivyo kufanya tangazo lako liwe la kuvutia zaidi na kuhamasisha wengine kukomenti.
3. Mfumo wa kiotomatiki wa kujibu na kulike komenti — jinsi ya kuseti mfumo unaolike na kujibu kila komenti masaa 24 kwa kila mtu anapomaliza kukomenti. Hii inawashawishi wateja kuona unajali na inachochea wengine kujiunga kwenye foleni ya kukomenti.
4. Kugeuza komenti kuwa mauzo — hatua kwa hatua jinsi ya kutumia majibu ya kiotomatiki kugeuza komenti kuwa wateja.
Kozi hii ipo katika mfumo wa video (za kiswahili) ambapo nakuonesha hatua kwa hatua ukiwa unaona mwenyewe jinsi ya kuseti na kurusha aina hii mpya ya sponsored ads zenye kuleta matokeo mazuri zaidi kwa sababu ya “Social Proof na FOMO”
Kwa nini nimefanya darasa liwe katika mfumo wa video? Kwa Sababu video ndio njia pekee rahisi ya kumfundisha mtu akiwa anaona kabisa anachotakiwa kufanya ukiachana na VITABU ambavyo hata huoni unachotakiwa kufanya na kuishia kusoma tu maandishi pasipo kujua jinsi ya kufanyia utekelezaji wa ambacho umekisoma.
Katika kozi hii ninakuonesha kabisa kwamba hapa unafanya hivi na hapa inakuwa hivi ukiwa unaona kabisa jinsi ninavyofanya. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi sana kwako kufanya utekelezaji wa haraka wa kile utakachojifunza na kufanya upate matokeo ya haraka hata kama huna uzoefu wowote wa masuala ya “IT”
Kozi Hii ya “Proof Ads Hack” Inagharimu kiasi Gani?
Kabla sijakwambia bei ya kujiunga kwenye kozi hii ningependa wewe mwenyewe ujipangie bei.
Unajipangia bei kiasi gani kwa kozi yenye kutoa mafunzo ambayo ni tiketi mpya ya kuitoa biashara yako kwenye kukosa wateja kuipeleka kwenye NEEMA ya kurusha matangazo ya kulipia endelevu yenye kuleta faida kubwa kila mwezi?
Unajipangia bei kiasi gani kwa kozi ambayo mafunzo yake yalinisaidia binafsi kutoka kwenye shimo kubwa la kupoteza hela nyingi kwenye matangazo ya kupilia mpaka kutengeneza faida ya 63,700,000 ndani ya siku 30 tu?
Unajipangia bei kiasi gani kwa kozi inayotoa mafunzo ambayo kwa hapa Tanzania sijaona mtu mwingine akifundisha kama ninachokifundisha?
Nadhani ukijipangia 500,000/= utakuwa upo sawa japokuwa ada hiyo bado ni ndogo sana ukilinganisha na faida ambazo unakwenda kuzipata kwa kufanya utekelezaji wa mafunzo haya.
Lakini unajua chakushangaza ni nini? Hutalipia hiyo 500,000/=
Pesa utakayolipia hata nusu ya hiyo laki 5 haifiki.
Hata Robo yake haifiki.
Nina mpango wa kuuza kozi hii kwa 100,000/=
Lakini kama utalipia kabla ya saa hiyo hapo juu kusoma sifuri, utajiunga kwenye kozi hii kwa gharama ya...
25,000/= Tu
Gharama ndogo ukilinganisha na pesa ambazo umeshazichoma kwenye matangazo bila kurudi.
Hata hivyo, saa hiyo hapo juu ikisoma sifuri bei inapanda mpaka 100,000/=
Lakini pia nakuzawadia bonasi zifuatazo kwa BURE kabisa kama utajiunga kwenye kozi hii ya Proof Ads Hack kabla ya saa hiyo hapo juu kusoma sifuri.
BONUS #1: Account Freedom Fix

Huenda kikwazo kikubwa cha wewe kushindwa kurusha matangazo kwa sasa ni akaunti yako ya matangazo kuwa “Restricted”
Usijali, bonasi hii lengo lake ni kutoa msaada kwako wa kufungua akaunti yako ambayo imefungwa.
Kwa hiyo akaunti kufungiwa sio kikwazo tena kwako kushindwa kurusha matangazo.
Thamani ya Bonus Hii ni 150,000/=
BONUS #2: Fresh Start Account Setup

Huenda kikwazo kikubwa cha wewe kushindwa kurusha matangazo kwa sasa ni akaunti yako kuwa na deni kubwa.
Usijali, bonasi hii lengo lake ni kutoa msaada kwako wa kufungua akaunti mpya ambayo haina deni ili usipoteze pesa nyingi kulipa deni ambalo halikukupatia faida yoyote.
Hii haimanishi nafuta deni. Deni huwa halifutwi. Kama mtu alikwambia anafuta madeni ni muongo. Kinachofanyika unafunguliwa akaunti mpya ambayo haina deni na hicho ndicho ambacho bonasi hii inakitoa.
Kwa hiyo kama akaunti yako ina deni kubwa, bonasi hii itakusaidia kuondoa kikwazo hicho ili uendelee kurusha matangazo bila deni.
Thamani ya Bonus Hii ni 150,000/=
Bonus zote 2 thamani yake kwa ujumla ni 300,000/= lakini ukijiunga kwenye kozi ya Proof Ads Hack unazipata zote kwa BURE kabisa.
Kwa hiyo kwa ujumla, hii hapa orodha ya vitu Vyote utakavyovipata kama utalipia leo:

Kozi ya Proof Ads Hack -Thamani yake 100,000/=
Account Freedom Fix -Thamani yake 150,000/=
Fresh Start Account Setup -Thamani yake 150,000/=
Jumla ya thamani: 400,000/=
Ofa ya Leo:
25,000/= Tu
Kwanini Natoa Punguzo La Bei Kubwa Sana Hivyo?
Kuna sababu 2 na ni rahisi kuzielewa.
1. Nashusha ngazi chini ili hata walio chini waweze kufika juu.
Tazama, mafanikio hayapatikani kirahisi.
Na hakuna mtu yeyote hapa chini ya jua ambaye anaweza akafanikiwa pasipo muunganiko wa juhudi binafsi na msaada kutoka kwa watu waliomtangulia.
Tunaishi Dunia ya “Saidiwa Usaidie”
Kuna maarifa nisingeweza kuyapata na nisingekuwa hapa nilipo leo hii endapo nisingepewa punguzo la bei na kushikwa mkono na walionitangulia.
Kwa hiyo mimi kupunguza bei ni kama kushusha ngazi chini ili ambao wanataka kupanda juu haraka iwe rahisi sana kwao.
2. Nahitaji uwe mteja wangu wa kudumu.
Tazama kwa kupunguza bei nina uhakika nitakuwa nimekuwekea urahisi wa kujiunga kwenye kozi hii.
Baada ya kujiunga kwenye kozi hii maarifa utakayopata lazima yakusaidie kuanza kurusha sponsored ads zenye kuleta matokeo mazuri zaidi.
Mpaka hapo nitakuwa nimeuteka moyo wako na...
Kwakua nina kozi zingine nyingi ambazo ninauza kwa hiyo nina uhakika utanunua maarifa tena na tena kutoka kwangu.

Kama baada ya kujiunga na kozi hii utakuwa hujalidhishwa na mafunzo yake (kwa sababu yoyote ile), wasiliana nami kupitia namba ya simu itakayokuwa kwenye risiti yako ya malipo — na nitakurudishia pesa zako zote bila swali wala kinyongo chochote.
Hata hivyo nina uhakika kabisa kwamba utaipenda kozi hii na utaridhika na kile nitakachokufundisha.
Kwanza nadhani wewe mwenyewe utashangazwa kwa kile ambacho naenda kukufundisha kwenye kozi hii.
Ukweli ni kwamba, unaenda kuwa mfanyabiashara wa tofauti kwa kurusha aina mpya ya sponsored ads yenye kutumia dhana yenye kuongeza mauzo inayotumiwa na makampuni makubwa sana duniani.
Kwa nini Ujiunge Kwenye Kozi Sasa Hivi na Sio Siku Nyingine?
Kwa ninavyoona mpaka sasa una machaguo matatu.
Chaguo #1: Unaweza kusahau yote niliyokuambia leo… na ukaendelea kufanya kile ambacho umekuwa ukikifanya siku zote na kupata matokeo yale yale ya siku zote.
Lakini kama ungekuwa unafurahishwa na matokeo unayoyapata kwenye sponsored ads zako, usingekuwa bado unasoma ujumbe huu.
Na bado unaendelea kusoma, hivyo hiyo inanihakikishia kuwa uko tayari kwa mabadiliko.
Kwa hiyo, kutofanya chochote hakuna maana kabisa. Lazima uchukue hatua.
Chaguo #2: Unaweza kunisahau na kuanza kutafuta kozi zingine.
Kila la kheri kwa chaguo hilo.
Kwa sababu ninachokufundisha kwenye kozi hii ni mfumo mpya na wa kipekee, wa kurusha sponsored ads tofauti na ambavyo walimu wote wa sponsored ads hapa Tanzania wanafundisha.
Watu hufanikiwa bila mfumo sahihi. Lakini si wengi. Kwa makadirio yangu, chini ya 1%. Lakini kama unakubaliana na uwezekano huo, fanya hivyo.
Kwa upande wangu, hiyo inaonekana kama njia isiyo faa.
Chaguo #3: Bonyeza hapa chini ujiunge kwenye kozi ya “Proof Ads Hack” na upate yote haya:
- Jinsi ya kutumia ads manager kuseti “Proof Ads” — aina mpya ya matangazo inayotumia nguvu ya Social Proof na FOMO kukuondoa kwenye ushindani sokoni na kuongeza uhitaji wa bidhaa yako machoni pa wateja.
- Maneno Maalum Ya Kukomenti —Haya ni maneno ambayo wateja wakikomenti kwenye tangazo lako, yanaongeza nguvu ya dhana ya “social Proof na FOMO” hivyo kufanya tangazo lako liwe la kuvutia zaidi na kuhamasisha wengine kukomenti.
- Mfumo wa kiotomatiki wa kujibu komenti — jinsi ya kuseti mfumo unaojibu kila komenti masaa 24 kwa kila mtu anapomaliza kukomenti. Hii inawashawishi wateja kuona unajali na inachochea wengine kujiunga kwenye foleni ya kukomenti.
- Kugeuza komenti kuwa mauzo — hatua kwa hatua jinsi ya kutumia majibu ya kiotomatiki kugeuza komenti kuwa wateja.
Na mengine mengi, mengi zaidi.
Wafanyabiashara watakao jiunga kwenye kozi ya Proof Ads Hack leo na kufanyia kazi kile kinachofundishwa wataanza kurusha sponsored ads zenye kuwapatia matokeo makubwa zaidi.
Swali pekee sasa ni, ‘Je, utakuwa mmoja wao?’
Kama uko tayari kwa mafanikio, bonyeza ‘LIPIA SASA’ hapa chini.Asante kwa kuchukua muda wako kusoma ukurasa huu, na natazamia kukutana na wewe darasani hivi karibuni!
Mr Bokko.
Copyright - Online Marketing System Pro | Privacy policy | Terms and conditions |
This site is not a part of the FacebookTM website or FacebookTM Inc. Additinally, this site is NOT endorsed by FacebookTM in any way. FACEBOOKTM is a trademark of FACEBOOKTM, inc.