Unaijua sababu moja pekee ambayo itamfanya networker mwenzako aachane na kampuni aliyopo aje ajiunge kwenye timu yako?
Kama huijui basi leo hii unaelekea kuijua sababu hiyo moja pekee.
Ukiijua sababu hiyo pekee basi utakuwa na uwezo wa kuwavuta networker wenzako kwenye team yako.
Sio kuwavuta tu –wao wenyewe ndio watakuwa wanakuomba uwaunge kwenye team yako.
Upo tayari nikwambie sababu hiyo pekee?
Twende kazi...
Kwenye post hii nimefundisha kwamba kuna makudi 2 tu ya watu ambao ndio prospects wako sahihi kushirikishwa fursa yako.
Kundi moja kati ya makundi hayo 2 ni networker wenzako.
Sasa inatakiwa utambue kwamba hakuna kundi gumu na kundi rahisi kama hili la networker wenzako.
Kumbuka watu hawa kama ni fursa wanayo tayari.
Kama ni bidhaa wanazo tayari kwenye kampuni waliyopo.
Unahisi wewe utawaambia nini ili waachane na kampuni waliyopo wakufate wewe kwenye team yako?
Utajigamba kwa uzuri wa bidhaa na mfumo mzuri wa malipo wa kampuni uliyopo?
Ukifanya hivyo networker mwenzako wataishia kukucheka.
Huwezi ukategemea kuwa na urafiki na mtu ambae unasifia kitu chako ilimladi tu chake kionekane kibaya.
Na hicho ndicho networkers karibia wote wanafanya.
Akili zao hazina utofauti na kasuku aliekalilishwa kusifia kampuni yake.
Nitakwambia sasa hivi... Nitakwambia badae... nitakwambia mara mia zaidi...
Kampuni uliyopo sio yako.
Najua ni ngumu kumeza ukweli ninaokwambia.
Lakini siku zote ukweli utabakia pale pale.
Kampuni uliyopo sio yako. Ni ya waanzilishi.
Labda nikuulize...
Mfumo wa malipo ukibadilishwa unahusishwa?
Bei za bidhaa zikibadilishwa unaambiwa utoe maoni yako?
Hapo ndo utajua kwamba kampuni uliyopo sio yako.
Ina wenyewe.
Kwahiyo kaa ukijua muda wowote siku yoyote ukivunja sheria zao huna chako.
Usinielewe vibaya.
Simaanishi hutakiwi kuwa proud na kampuni uliyopo. Hapana.
Lazima uwe proud kwa kampuni uliyopo lakini kuwa proud kusikufanye ujisahau nakuona kampuni ni yako.
Kwahiyo achana na habari za kuitangaza kampuni ambayo sio yako.
Ohoo nimeanza sasa kuhubiri badala ya kuendelea na maada yetu ya leo.
Kwanini hujaniambia lakini kama naenda nje ya maada ya leo.
Sijui hata nilikuwa nimeishia wapi.
Ahaa nimekumbuka nilikuwa nimeishia pale kwamba huwezi ukamfanya networker mwenzako ajiunge kwenye team yako kwa kusifia kampuni yako na kuiponda kampuni yake.
Hiyo sio njia sahihi.
Njia sahihi ni ipi sasa? Subiri nitakwambia hapo mbele kidogo.
Tazama...
Kwa networker ambae yupo active kwenye kampuni yake lazima anatafuta watu wakujiunga kwenye team yake.
Tatizo ni kwamba njia ambazo anazitumia kupata watu hao wakujiunga kwenye team yake hazimpatii matokeo mazuri.
Zinamfanya azidi kuhangaika siku hadi siku na kuiona biashara ngumu.
Hivyo basi networker huyu anahitaji njia tofauti kabisa ya kumsaidia kupata watu wa kujiunga kwenye team yake.
Kwahiyo kama wewe utaweza kuwa na njia hii ya tofauti ya kumsaidia networker huyu kupata watu wa kujiunga kwenye fursa yake pasipo msoto na mahangaiko anayoyapata kwa sasa basi kazi imeisha.
Networker huyo lazima atakufata wewe kwenye team yako kwasababu ya wewe kuwa na njia hiyo bora yenye kumsaidia kupata watu wa kujiunga kwenye team yake bila mahangaiko anayoyapata kwa sasa.
Ukiweza tu kuwa na njia ambayo inaweza ikawasaida networkers kupata watu wakujiunga kwenye fursa pasipo mahangaiko na msoto wanaoupata kwa sasa basi networkers wote utakaowataka wajiunge kwako watakufata wao wenyewe na kuomba wawe kwenye team yako.
Na hiyo ndo sababu moja pekee ya kumfanya networker mwenzako aachane na kampuni aliyopo akufate wewe kwenye team yako.
Huwezi ukataka networker mwenzako aje ajiunge kwako wakati njia unazozitumia kupata watu wakujiunga kwenye fursa ndio zilezile sawa na ambazo anazitumia yeye ambazo hazimpatii matokeo.
Lazima uwe na kitu cha tofauti.
Nimemaliza.
Let’s call it a day.
Ni mimi,
Mr Bokko.
P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.
P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.