unajua kupata watu wakujiunga kwenye fursa yako hakuna utofauti na kuchumbia?
Ni kweli.
Kwasababu ili mtu ajiunge kwenye team yako lazima akukubali kwanza halafu ndo biashara ifate.
Vivyo hivyo kwenye mapenzi –ili upate mpenzi lazima ukubalike kwanza ndio uchumba ufate.
Kwahiyo mapenzi hayana utofauti na kuuza na kununua.
Mtu asipoona cha kununua kwako sahau kabisa mtu huyo kuwa mpenzi wako.
Kwa lugha rahisi mtu asipoona una sifa anazozitaka sahau kabisa kuhusu kuwa wapenzi.
Iko hivi...
Siku zote mtu ananunua bidhaa anayoipenda na ambayo anaona inamfaa yeye.
Kwahiyo usifanye kosa hata siku moja –kuchumbia hakuna utofauti na kuuza na kununua.
Na pia kuingiza watu kwenye fursa hakuna utofauti na kuchumbia.
Nisikilize kwa makini... (Hivi unaweza ukasikiliza maandishi?)
Nisamehe. Nakutania tu buana.
Haya tuendelee...
Linapokuja suala la marketing kitu cha msingi sana ni bidhaa unayouza.
Lazima uwauzie watu kitu wanachokitaka wao na sio unachokitaka wewe.
Kama unawauzia watu bidhaa ambayo hawaitaki hata ufanye nini hata siku moja hakuna mtu atanunua bidhaa yako.
Tazama...
Unaweza ukawa na chakula kitamu sana dunia nzima lakini kama hakuna mtu mwenye njaa chakula chako utakila mwenyewe.
Kama huamini ngoja nikutolee mfano mmoja.
Ebu fikiria umeenda kwenye party...
Halafu kwenye party hiyo ukakutana na mtoto mzuri balaa yani ni anawaka (a.k.a pisikali) ambaye kila mwanaume aliyehudhuria kwenye party hiyo anataka kuwa na mahusiano naye.
Baadhi ya wanaume wanamfata wanamwambia niwaigizaji kwahiyo akiwa na mahusiano nao watamfanyia nae mpango awe muigizaji ili anze kutengeneza hela lakini wapi pisikali hii bhana Haina shobo kabisa na masuala ya kuigiza.
Wengine wanamfata na kumwambia ni waandishi wa habari za magazetini kwahiyo akiwa na mahusiano nao watamuweka kwenye kurasa za mbele za magazeti yao hivyo kumfanya awe maarufu lakini wapi pisikali ikawatolea nje Maana haina shida na umaarufu wowote.
Wengine wanamfata wanamwambia ni watoto wa matajiri, Wana makampuni makubwa, Wana mali nyingi, magari ya kifahari kwamba mtu yeyote mwenye mahusiano nao hatakuwa na shida tena na hela kwamba suala la kukosa hela litakuwa kicheko kwake...
Lakini chakushangaza ni kwamba mtoto huyo mzuri akawatolea nje na wenye pesa zao.
Wengine sasa ambao hawana hela lakini wanajidai kwa visura vyao vyakuvutia (eti handsome boys kumbe kenge tu) wakamfata wakijinadi kwa uzuri waliokuwa nao kwamba kwa uzuri aliokua nao wakiwa na mahusiano naye wanaendana Sana lakini mtoto mzuri huyu anaishia kuwacheka.
Akaja kijana wa mwisho. Hela Hana. Uzuri Hana. Bwege fulani hivi. Yani hana mvuto wa aina yoyote akamfata mtoto mzuri na kumnong'oneza maneno fulani.
Ikasikika sauti kubwa kutoka kwa mwanadada...
"Ndio ndio twende zetu"
Yule mtoto mzuri akamushikilia mkono yule jamaa wakasepa zao.
Unadhani kwanini jamaa huyu alimkamata mtoto mzuri huyu wakati wengine wote walishindwa?
Jibu ni rahisi.
Huyu jamaa alifahamu mtoto mzuri alichokuwa akikihitaji Kwa wakati huo, hivyo alitoa maelezo ambayo yalionesha kupitia yeye mwanadada atapata hitaji lake ndio maana aliwashinda wengine wote.
Jamaa aligundua kwamba mwanadada ni teja kwahiyo alichomnong'oneza ni hiki...
oya sikia Nina kete zangu hapa nimezipata mtaa fulani ivi, vipi upo tayari tukapige tupandishe zetu stimu na mizuka?
Mwanadada kwakuwa ni teja aliguswa penyewe.
Alikuwa Hana ujanja. Alichokuwa anahitaji nikupata stimu na mizuka ili party iende vizuri yani!
Kwahiyo hata kwenye Suala zima la kupata watu wakujiunga kwenye fursa yako...
Inatakiwa ujue ni kitu gani uwauzie au uwambie prospects wako ili iwe rahisi kwao kuipenda fursa yako.
Asante.
Ni mimi,
Mr Bokko.
P.P.S: Kama una swali lolote au una cha kusema kuhusu post hii usisahau kukoment hapo chini.
P.P.S: Kama ungependa kujifunza namna ya kutumia matangazo ya kulipia Facebook na Instagram kupata wateja wengi bofya hapa kupata maelezo zaidi.